March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ishara ya kidole cha mwisho kumponza Mourinho

Jose

Spread the love

KOCHA mkuu wa Manchester Unite Jose Mourinho yupo katika wakati mgumu tena baada ya Chama cha Mpira wa Miguu England (FA) kumchunguza kufuatia kuonesha ishara ya kidole cha mwisho mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu uliopigwa Old Trafford na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle United. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea)

Mourinho alionesha ishara hiyo alipokuwa akitoka uwanjani mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo huku akiwa anatamka maneno kwa lugha ya kireno ambayo yaliyo tafsiliwa na kuonekana kama matusi yalionekana kuwalenga magwiji wa klabu hiyo Paul Scholes na Rio Ferdinand ambao walinukuliwa wakisema kocha huyo anahalibu timu hiyo.

Hata alipoulizwa na waandishi wa habari nini maana ya kuonesha ishara ile, alisema kile ni kidole tu na ndio kifupi kuliko vyote.

Hii ni mara ya tatu kwa kocha huyo kuoneasha ishara hiyo ya kidole katika matukio tofauti, alionekana akifanya hivyo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Valencia uliomalizika kwa sare ya bila kufungana na mara ya pili akiwa kwenye gari yake binafsi na kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle.

Kocha huyo amekuwa katika wakati mgumu wa kunusuru kibarua chake ndani ya klabu hiyo kutokana na kuwa na mwenendo mbovu wa matokeo huku sababu kubwa ikiwa ni migogoro na wachezaji sambamba na mkurugenzi wa timu hiyo Ed Woodward ambaye alikataa kumpa fedha za kutosha kwenye dirisha la usajili.

error: Content is protected !!