December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Isaac Gamba afariki dunia

Spread the love

ALIYEWAHI kuwa Mtangazaji wa Radio One na ITV, ambaye baadaye alijiunga na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW), Isaac Gamba amefariki dunia mjini Bonn Ujerumani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mtangazaji huyo amekutwa amefariki nyumbani kwake na bado sababu za kifo chake hazijajulikana.

Taarifa za kifo cha Gamba zinasema kuwa marehemu hakutokea kazini kwake tangu siku ya Jumatatu hivyo wafanyakazi wake walianza kujenga mashaka ndiyo walipolazimika kumfuata anapoishi.

Imeeleza kuwa walipofika nyumbani kwake walikuta nyumba imefungwa ndiyo walipolazimika kuvunja mlango na kukuta amefariki.

error: Content is protected !!