July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

IS yashukiwa na mvua ya mabomu

Ndege ya kivita ya Marekani

Spread the love

Ndege za kivita za Marekani zimefanya mashambulizi ya mabomu dhidi ya inayojiita Dola ya Kiislamu (IS).

Mashambulizi hayo siyo tu yanatoka angani bali ngege za Marekani zimefanya pia mashambulizi huko Iraq na Syria kutoka kwenye meli zilizopo eneo la ghuba ya Uajemi.

Aidha, kuanzia Agosti 8 hadi 26, ndege za Marekani zilifanya mashambulio 216 ndani ya Iraq mashumbulio 41 huko Syria. Mashabulizi hayo yalifanywa kutoka angani.

Generali Martin Dempsey, mkuu wa jeshi la Marekani amesema kuwa IS inasambaratishwa na mashambulizi kutoka angani. Hata hivyo mashambulizi ya angani peke yake hayatoshi.

Dempsey amesema kuwa mazungumzo na uwepo wa askari wa ardhini vinahitajika. Kwa mujibu wa Dempsey askari wa miguu 15,000 watahitajika kwa ajili ya jeshi la ardhini huko Syria.

Nchi za Ulaya zimekubaliana kushambulia maeneo yaliyopangwa kama ilivyoombwa na serikali ya Iraq. Wakati huo huo ndege za Marekani, Saudia na Falme za Kiarabu zimekuwa zikishambualia maeneo ya mashariki mwa Syria, mashambulizi yaliyoelekezwa pia kwenye maeneo ya visima vya mafuta.

“Itahitajika nguvu tofauti zaidi ya mashambulizi ya angani kuweza kukamata maeneo ya Syria na Iraq yanayokaliwa na IS. Nguvu hizi ni askari wa miguu na hawapaswi kuwa wamarekani. Hawa wanapaswa kuwa wa Iraq na wa Kurd pamoja na wapinzani wa Syria wenye msimamo wa kati”, alisema Dempsey.

Siku ya Ijumaa Uingereza imekubali kuiunga mkono Marekani kwa kufanya mashambulizi ya angani. Wakati huo huo ndege za Ufaransa tayari zipo na zimeshaanza kufanya mashambulizi, huku Ubeligiji na Uholanzi kila moja imeahidi kuchangia ndege za aina ya F-16 na Denmark imeahidi kupeleka ndege saba.

Akizungumza kutoka Pentagon Dempsey amesema mashambulizi ya wiki hii yamevuruga kabisa uendeshaji wa shughuli za IS ikiwa ni pamoja na ugavi, uongozaji na utoaji maagizo. Takribani nchi 40 ikijumuisha nchi kadhaa za Mashariki ya Kati zimeungana na Marekani.

error: Content is protected !!