Serikali ya Irani, imemnyonga aliyekuwa Naibu Waziri wa Ulinzi wa Irani,Alireza Akbari, kwa kosa la kutoa siri za nchi hiyo na kufanya ujasusi kwa ajili ya Uingereza. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, taarifa za kunyongwa kwa Akbari zilitolewa na chombo rasmi cha habari cha Mahakama ya Irani, Mizan, bila kutaja tarehe ambayo raia huyo wa Iran pamoja na Uingereza alinyongwa.
Mitandao ya kimataifa imeripoti kuwa, Familia ya Akbari iliitwa kwenda kumuaga kwa mara mwisho katika gereza alilokuwemo, Jumatano ya wiki hii.
Akbari alikamatwa 2019 na mamlaka za Iran kisha alikutwa na hatia ya kufanya ujasusi kwa ajili ya Uingereza, tuhuma ambazo alikana kuzifanya.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, amelaani tukio hilo na kudai kuwa kitendo cha Iran kumnyonga Akbari ni cha kinyama kinachooashiria utawala mbaya usioheshimu haki za binadamu, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, James Cleverly akisema hukumu hiyo lazima ipingwe.
Leave a comment