October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Iran yalianzisha, yashambulia kambi za Trump

Spread the love

VIASHIRIA vya Vita ya Tatu vya Dunia tayari vimedhihiri, Iran imeanza kutekeleza kile ilichoahidi kwamba, itashambulia Marekani kulipiza kisasi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Ni baadaya ya Jeshi la Marekani kumuua kiongozi wa juu wa Jeshi la Iran, Qasem Soleimani, tarehe 3 Januari 2020. Mazishi ya Soleimani yamefanyika jana tarehe juzi tarehe 6 Januari 2020.

Kambi mbili za Marekani zilizoshambuliwa na Iran nchini Iraq zipo katika Mji wa Irbil na Al Asad.

Televisheni ya Taifa ya Irani imetangaza kwamba, shambulio hilo ni utekelezaji wa ahadi Irani ya kulipa kisasi dhidi ya Marekani, baada ya nchi hiyo kumuuwa Qasem Soleimani, aliyekuwa kiongozi mwandamizi wa jeshi la nchi hiyo.

Shambulio hilo lilifanyika jana tarehe 7 Januari 2020, saa kadhaa baada ya Irani kumzika Jenerali Soleiman.

Jeshi la Ulinzi la Iran limeonya nchi washirika wa Marekani, wanaohifadhi vikosi vya jeshi vya nchi hiyo, kutoingilia mgogoro huo.

Donald Trump, Rais wa Marekani, amesema wanafanya tathmini ya majeruhi pamoja na uharibifu uliotokana na shambulio hilo, na kwamba watatoa tamko kuhusu suala hilo, kesho tarehe 9 Januari 2020.

“Kila kitu kipo sawa, Kambi zetu mbili za Jeshi la Marekani zilizopo Iraq zimeshambuliwa na Iran, tunafanya tathmini kujua kama kuna waliopata madhara au uharibifu wowote wa mali, yote kwa yote tuna vifaa Bora vya kivita kuliko Nchi yoyote Duniani, nitatoa tamko hivi punde,” amesema Trump.

Hata hivyo, Rais Trump amesema kwa kejeli kwamba, hatua hiyo ya Irani kushambulia kambi zake ni nzuri, na kutishia kwamba, Marekani ina nguvu za kijeshi na dhana za kivita kila mahali duniani.

error: Content is protected !!