October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Iran kuruka vikwanzo vya kibiashara

Spread the love

Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran inatarajia kupata afueni kwa kufunguliwa milango ya kibiashara baada ya kutimiza mashatri ya Umoja wa Kimataifa (UN).

Hatua hiyo inatokana na kuwepo kwa taarifa kwamba, taifa hilo limesitisha uzalishaji wa mabomu ya nyuklia jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele na umoja hupo pamoja na nchi zilizoendelea.

Taarifa ya usitishwaji huo imeelezwa na shirika la uangalizi wa masuala ya nyuklia la kimataifa (IAEA) na kwamba, matumizi hayo ya nyuklia yataelekezwa kwenye uchumi zaidi.

IAEA inatarajiwa kutoa taarifa yake juu ya ukweli kuwa Iran imesimamisha uzalishaji wa mabomu ya nyuklia kwenye vinu vyake na makuabaliano ya Serikali ya Tehran ya kuwekeza zaidi nyuklia kwenye matumizi ya amani.

Iran imekuwa ikikosa mamilioni ya dola kwa kufungiwa kufanya mauzo ya mafuta yake kutokana na kuwekewa vikwazo kwa sababu ya muendelezo wake wa unurishaji wa vinu vya nyuklia.

Tayari Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry amewasili mjini Vienna ambapo anatarajiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif ambaye pia amefika mjini hapo.

Hata hivyo, ulimwengu umepokea vizuri mazungumzo ya IAEA kuhusu kufungamana Iran na ahadi zake katika mapatano ya nyuklia sambamba na taarifa ya pamoja ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya.

Shirika la Habari la Itar Tass la Russia limetangaza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi amesema mafanikio katika mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) kati ya Iran na madola sita makubwa duniani ni jambo ambalo litadhamini usalama wa Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.

Shirika la AFP nalo limemnukulu Laurent Fabius, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa akisema mapatano ya nyuklia ya Iran ni ushindi mkubwa wa kidiplomasia.

Associated Press imemnukulu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA akisema utekelezwaji wa mapatano wa nyuklia ni mwanzo mpya.

error: Content is protected !!