April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ingizeni wake zenu – Zungu

Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala

Spread the love

MUSSA Zungu, Mbunge wa Ilala, amewataka maofisa na askari magereza kulinda heshima ya nyumba za serikali waliokabidhiwa, kwa kuhakikisha wanaingiza wake zao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya majengo 12 ya nyumba za askari hao zilizoko Ukonga, jijini Dar es Salaam leo tarehe 23 Januari 2020, Zungu amewataka kuingiza wake zao kwenye nyumba hizo.

Zungu amesema, nyumba hizo zimeombewa dua na mashekhe, mapadri pamoja na maaskofu, hivyo wanatakiwa kuwa waadilifu katika matumizi ya nyumba hizo.

“Nyumba hizi zimeombewa dua na masheikh na baba paroko. Na mtu atakayeingia kwenye nyumba hizi, dua hii ina maana muwe waadilifu. Mkiingia humu ndani ingizeni wake zenu ili kuwe na heshima kwa aliyejenga aliyetoa pesa na heshima ya kiti cha uraisi,” amesema Zungu.

Majengo hayo  anayokabidhiwa Rais John Magufuli,  majengo manne ni ya maafisa wa jeshi la magereza na nane kwa ajili ya maaskari wa kawaida.

error: Content is protected !!