Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Infinix, Vodacom kuwanufaisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu kupitia Hot 30
Habari Mchanganyiko

Infinix, Vodacom kuwanufaisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu kupitia Hot 30

Spread the love

KAMPUNI ya Vodacom kwa kushirikiana na Infinix leo wametangaza uzinduzi wa simu mpya ya Infinix toleo la HOT  30 pamoja na kampeni ya chemsha bongo ya Tech/Tech quiz  inayohusisha wanafunzi wa vyuo vikuu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Vodacom imekuwa na maono ya kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali na hadi sasa, kampuni hiyo ina nia ya kutoa simu janja zenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu kwa kila Mtanzania. Hii ndiyo motisha ya ushirikiano wake na Infinix ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu wanaweza kuwa washiriki hai wa jumuiya ya kidijitali ambayo nchi inaijenga kwa uchokozi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, George Lugata amesema, “Vodacom ina historia kubwa katika uendelezaji na uongezaji wa upatikanaji wa huduma za kiteknolojia kupitia simu. Tunaishi katika ulimwengu unaotaka kutuunganisha pamoja ambapo simu za kisasa sio anasa tena; bali nihitaji muhimu la kiuchumi. Simujanja huwawezesha watu kuwasiliana, kujenga urafiki na pia kunufaika na fursa kadha wa kadha zinazotuzunguka ukilinganisha na kipindi cha nyuma.”

Lugata aliongeza kuwa Vodacom, inaamini kuwa kila mtu anastahili kumiliki simujanja zenye ubora na ndio sababu kampuni hiyo inakuja na vumbuzi mbalimbali ili kumuwezesha kila Mtanzania kumiliki simujanja.

Aliendelea kuwa kampuni itawazawadia wateja watakaonunua simu hii 96GB kwa muda wa miezi 12 ili kufurahia huduma za kidijitali zinazotolewa na Mtandao Supa.

Kukuza udadisi na kushirikishana maarifa miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu, Vodacom kwa kushirikiana na Infinix wataendesha ‘Chemsha Bongo kwa vyuo vinne vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Lugata ameonesha kujivunia ukurasa mpya wa upatikanaji wa simu nafuu ambazo wamezindua kwawateja na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidikupitia Mtandao Supa ambapo kwa sasa unaendesha kampeni ya ‘Zaidi ya Mtandao’ iliyojikita katika kudhihirisha utoaji wa huduma na bidhaa zenye manufaa kwa Watanzania wote nchini.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Infinix, Eric Mkomoya amesema kuwa, “Infinix ni kampuni yenye mafanikio inayojulikana kimataifa na wana furaha kuwatangazia ujio mpya wa Infinix HOT 30 yenye maboresho ya hali ya juu kwa wapenzi wa michezo na burudani za kwenye simu ikiwa imekuja na ‘8-core Helio G88 chip’ ikiwa na ‘ARM Cortex-A75 cores’mbili zenye nguvu kufanya kazi kwa kasi ya juu mpaka kufikia 2.0GHz.

Pia ina teknolojia bunifu ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi vitu, kutoka 8GB iliyonayo mpaka kufikia 16 GB. Matokeo yake inawezesha kuwaka kwaharaka na uwezo wa kuruhusu applikesheni zingine kufanya kazi, kuwapatia watumiaji urahisi wa kutumia kwa ufanisi bila kuathiri matumizi mengine.”

Mkomoya alifafanua kuwa Infinix HOT 30 imekuja nateknolojia ya kuchaji ya 33W yenye betri yenye uwezo wa5000mAh hivyo kufanya kikomo cha matumizi ya betri kuendelea kudumu kwa muda mrefu. Imekwishafanyiwa majaribio kuona betri ya simu itadumu kwa muda gani kupitia programu tofauti maarufu kama vile za filamu, michezo na burudani, na video fupi huku ikiwa na ufanisi kwenye picha angavu, simu hii ina 90Hz ambayo huboresha matumizi mara kwa mara ili mtumiaji aendelee kufurahia.

‘Chemsha Bongo kwa wanafunzi wa vyuo vikuuitaendeshwa kwa muda wa wiki nne ambapo washindiwataondoka na simu za Infinix HOT 30. Kwa kuongezea, wataweza kununua simu hizi mpya kwa punguzo la bei ndani ya kipindi ambacho ya zoezi hili kwenye maeneo yao ya vyuo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!