WIZARA ya mambo ya Nje ya India (MEA) imetoa hadhari juu ya hali ya mwenendo wa ugonjwa wa Uviko-19 nchini China pamoja na wasiwasi wa hatua za kujikinga zinazochukulia na nchi hiyo na kuongezeka kwa kesi mpya za ugonjwa huo. Imeripotiwa na Shirika la Habari la ANI News Service … (endelea).
Mapema wiki hii, Msemaji wa Wizara hiyo, Arindam Bagchi alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari alisema, India ikiwa kitovu cha dawa duniani haitaacha kuzisaidia nchi nyingine zisikumbwe na ugonjwa huo ikiwa pamoja na kutoa tahadhari.
“Tunaangalia hali ya Covid nchini China. Daima tumesaidia nchi nyingine kama duka la dawa duniani, Bado hatujatoa ushauri wa kusafiri lakini watu wanapaswa kufuata miongozo ya ndani katika nchi wanayoishi,” alisema Msemaji wa MEA Bagchi.
Kwa mujibu wa Chombo cha habari cha ANI, Siku ya Jumatano, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus alielezea wasiwasi wake juu ya hali inayoendelea nchini China, na ripoti zinazoongezeka za ugonjwa mbaya.
“Ili kufanya tathmini ya kina ya hatari ya hali hiyo, WHO inahitaji maelezo ya kina zaidi juu ya ukali wa ugonjwa, kulazwa hospitalini na mahitaji ya msaada wa kitengo cha wagonjwa mahututi.
“WHO inaunga mkono China kuelekeza juhudi zake katika kutoa chanjo kwa watu walio katika hatari kubwa zaidi nchini kote na tunaendelea kutoa msaada wetu kwa huduma za kliniki na kulinda mfumo wake wa afya,” alisema mkuu huyo wa WHO.
Uchambuzi wa Airfinity unakosoa jitihada ndogo za China kwenye kukabiliana na ugonjwa huo kwa hoja kuwa nchi hiyo inaviwango vidogo vya kinga kulinganisha na idadi ya watu wake. Raia wake walichanjwa na jabs zinazozalishwa na Sinovac na Sinopharm ambazo zimethibitishwa kuwa na ufanisi mdogo na kutoa kinga kidogo dhidi ya maambukizi na vifo.
Leave a comment