Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa India kuizidi kete China kuiongoza G20
Kimataifa

India kuizidi kete China kuiongoza G20

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi
Spread the love

 

USHAWISHI ya Taifa la India imezidi kuongezeka katika anga ya kimataifa hasa pale ilipoungwa mkono kuogoza G20. Imeandikwa na The Interpreter … (endelea).

G20 ni mkutano mgumu zaidi barani Asia. India imechukua jukumu hilo la kuwa mwenyekiti wa mkutano huo ulioandaliwa na Indonesia jijini Bali mwishoni mwa mwaka jana 2022.

Mkutano huo ulijadili ajenda nzito ikiwemo vita ya Ukraine na Urusi, mivutano kati ya mataifa makubwa kuhusu deni, nishati, chakula, mfumuko wa bei, biashara na teknolojia.

Ni wazi kwamba New Delhi pia ilihesabu kwamba licha ya hali ngumu, kuna uwezekano wa kupata faida za kidiplomasia katika kuongoza G20.

New Delhi ilikuwa na nia ya kuchukua kazi hiyo. Huku uchaguzi mkuu ukingoja mwaka wa 2024, serikali ya Narendra Modi bila shaka iliona fursa ya kuwaeleza wapiga kura kwamba India sasa inaheshimika duniani kote.

India ilipata fursa ya kuongeza ushawishi wake katika Global South na kujiweka kama daraja kati ya Magharibi na nchi zinazoendelea.

Modi na Waziri wake wa mambo ya nje mwenye juhudi sawa, Subrahmanyam Jaishankar, walipiga simu kwa wenzao  kutafuta maoni kuhusu kile ambacho G20 kinaweza kufanya kwa ajili ya nchi zao.

Sambamba na hilo, India iliwasilisha pendekezo la kuongeza Umoja wa Afrika kwenye kongamano hilo, ambalo liliidhinishwa katika mkutano huo.

Pili, New Delhi ilitathmini miradi mingi ilizinduliwa kando ya mkutano wa viongozi. Jambo la kuvutia macho zaidi ni mpango uliokubaliwa na Umoja wa Ulaya, Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Marekani kufadhili na kujenga kinachojulikana kama Ukanda wa Kiuchumi wa India-Mashariki-Ulaya (IMEC) unaounganisha India na Ghuba.

Modi alizindua ni Muungano wa Global Biofuel Alliance, pamoja na viongozi wa Argentina, Bangladesh, Brazil, Italia, Mauritius, Singapore na Marekani, ambao unalenga kuendeleza na kukuza nishati endelevu ya mimea.

Ushindani wa kimkakati kati ya China na India umeongezeka tangu Xi Jinping aingie madarakani mwishoni mwaka 2012.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

Kimataifa

Uvamizi wa kijeshi Milango ya bahari ya Taiwan G7 yapinga China

Spread the loveMKUTANO wa Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi za...

error: Content is protected !!