July 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ilala yatenga 138 Bil kuboresha elimu

Spread the love

CHARLES Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam amesema, Baraza la Madiwani la Ilala limepanga kutumia takribani Sh. 138 Bilioni kwa ajili ya kuboresha elimu katika manispaa hiyo, anaandika Happyness Lidwino.

Kuyeko amesema hayo wakati akizungumza na mtandao huu na kwamba, fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuboresha kwenye maeneo ya shule zenye uhitaji.

“Wakati nikifanya ziara zangu za kikazi, niligundua kuwa shule nyingi Ilala zina uhitaji  hususani wa madarasa, madawati, vyoo, maji na viwanja vya michezo. Mimi pamoja na madiwani wangu tumejiridhisha hilo na tutalifanyia kazi,” amesema Kuyeko.

Akitaja baadhi ya shule ambazo zinauhitaji mkubwa wa madawati na madarasa amesema ni Shule ya Msingi na Sekondari ya Mabwepande, Shule ya Sekondari Vingunguti.

“Tumepanga bajeti hiyo bila kuwa na pesa mkononi lakini tunatarajia kuipata kutokana na mapato ya wilaya hii. Hadi sasa tayari tumeaza ukusanyaji wa mapata ambapo kwa mwaka huu tunatarajia kukusanya Sh. 85 Bilioni.

error: Content is protected !!