July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ilala wataonja tofauti kuchagua Chadema

Spread the love

CHARLES Kuyeko, Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, ameahidi kuwatumikia wananchi kwa bidii ili waweze kubaini tofauti kuwa waliwahi kutumikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaandika Happyness Lidwino.

Kuyeko ametoa ahadi hiyo Jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa Katiba na Ilani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Kasmir Mabina Mratibu wa Chadema Kanda ya Pwani kwa niaba ya chama.

Mabina amesema lengo la chama kumkabidhi ilani hiyo ni kumuongoza katika utendaji wake pasipo kuingiliwa na chama.

Amesema, ndani ya ilani hiyo kuna vipaumbele vya aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na wabunge. Mabina amemwambia Meya huyo atekeleza vipaumbele hivyo.

Vipaumbele ambavyo wamemtaka kuanza navyo ni pamoja na, elimu bora, makazi ya wananchi pamoja na kusimamia mapato yatokanayo kwenye Manspaa yake.

Kwa upande wake Kuyeko baada ya kuipokea ilani hiyo amesema, tayari ameaza utekelezaji kwenye baadhi ya shule zilizopo kwenye eneo lake kwa kuboresha miundo mbinu.

“Nimeshaenda Bonyokwa, Ukonga na Pugu nimeona changamoto zilizopo na nimeshachukua hatua za utekelezaji kwa kushirikiana na madiwani.” amesema Kuyeko.

Hata hivyo, amesema amejipanga kuboresha elimu kutokana na mapato anayotarajia kukusanya kuanzia mwezi ujao ambapo amebainisha vyanzo vya mapato anavyotarajia ni, mabango yote, Majengo kwa kukusanya kodi na Masoko kwa kukusanya ushuru.

“Ilala ni moja kati ya eneo lenye biashara nyingi hivyo natumaini kupitia kodi tutapata fedha nyingi zitakazopatikana na kutekeleza matakwa ya wananchi Ilala hasa suala la elimu bure.Tayari nimeanza hatua za kuongeza madarasa matano katika kila shule,” amesema Kuyeko.

error: Content is protected !!