July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ilala kukusanya bilioni 58/-

Afisa uhusiano wa manispaa ya Ilala wa kwanza (kushoto) akizungumza na waandishi

Spread the love

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imepanga kukusanya Sh. 30 bilioni kutoka vyanzo vyake vya ndani, ambavyo ni kodi ya majengo, leseni za biashara, ushuru wa mabango na kodi ya huduma jiji. Anaadika Sarafina Lidwino… (endelea)

Kwa mujibu wa Afisa uhusiano wa manispaa hiyo, Tabu Shaibu, hadi sasa wameshakusanya Sh.21 bilioni (sawa na asilimia 73) ya lengo la mwaka.

Shaibu amesema, katika mwaka wa fedha 2015/2016, wamepanga kukusanya Sh. 58 bilioni kutoka kwenye vyanzo hivyo na kwamba mchakato wa ukusanyaji wa takwimu za majengo na leseni za biashara uliaza 8 Aprili mwaka huu, na utadumu kwa miezi mitatu.

Ameeleza kuwa, lengo hilo ni kuweza kupata takwimu sahihi za wakazi, wamiliki wa majengo ya biashara na makazi pamoja na wafanyabiashara wa manispaa hiyo.

“Takwimu hizo zitatumika kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wetu na kuweka uhusiano wa karibu kwani mteja akikata leseni, tayari anakuwa ameingia kwenye mfumo wetu,”amesema Shaibu.

Shaibu ameongeza kazi hiyo itatekelezwa na watumishi wa manispaa pamoja na wasaidizi wao vijana wapatao 300 walioajiliwa.

Hata hivyo, Shaibu amewataka wanachi kuwa makini katika kazi hiyo na kutoa ushirikiano kwa watumishi hao watakapopita kukusanya takwimu hizo.

error: Content is protected !!