Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ikosoeni serikali – Rais Samia
Habari za Siasa

Ikosoeni serikali – Rais Samia

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

MAMA Samia Suluhu Hassan, Rais wa Awamu ya Sita wa Tanzania, amewataka wabunge kuikosoa serikali yake, pale inapofanya vibaya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Rais Samia amesema hayo leo Alhamisi tarehe 22 Aprili 2021, akihutubia Bunge, jijini Dodoma.

Katika hotuba yake hiyo aliyoitoa kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021, Rais Samia amesema, mawaziri wake wakifanya vibaya wakosolewe vikali.

“Naomba bunge kutoa ushirikiano mkubwa kwa serikali, tukosoeni pale inapobidi na naomba mtukusoe vikali sana. Mawaziri wangu wakileta vitu visivyoeleweka wakosoeni vikali sana, lakini wakosolewe katika lugha ya kibunge,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema Serikali yake iko tayari kupokea ushauri wa wabunge na Watanzania kwa ujumla wenye nia ya kuleta maendeleo ya nchi.

“Na mimi nataka niwaahidi kuwa Serikali itakuwa tayari wakati wote kupokea ushauri wenu, lakini pia wa wengine wanaotaka kuiletea maendeleo nchi yetu,” amesema Rais Samia.

Mama Samia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Tano, amerithi mikoba ya Hayati Dk. John Magufuli, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021, akiwa madarakani.

Dk. Magufuli alifariki dunia kwa ugonjwa wa mfumo wa umeme wa moyo, kwenye Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, kisha mwili wake ulizikwa nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!