August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ICC itabaki salama?

Spread the love

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) itabaki salama? Ni swali linaloweza kuibuka baada ya Nchi za Afrika kuunda mkakati wa kujitoa katika mahakama hiyo, anaandika Wolfram Mwalongo.

Msukumo wa mataifa hayo kufanya mkakati huo unatokana na kile kinachoitwa, kuonewa na mahakama hiyo kwamba, ina lenga zaidi viongozi wa Afrika.

Baada ya mataifa ya Kenya, Burundi na Afrika Kusini kutangaza wazi kujitoa (ICC), Gambia nayo imetangaza kufuata njia hiyo huku ICC ikionesha kusikitishwa na uamzi huo.

Afrika imekuwa katika mgogoro wa muda mrefu na ICC kwa madai, imekuwa ikiendesha shughuli zake kwa uonevu hasa kwa kuwaburuta viongozi wa Bara la Afrika pekee.

Hata hivyo, yowe dhidi ya mahakama hiyo lilianza katika Umoja wa Afrika (AU) wakati Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe alipokuwa mwenyekiti.

Ingawa hakukuwa na sauti ya wazi wakati huo, sasa kumekuwa na kampeni za chini kwa chini kushinikiza kuisusa ICC.

error: Content is protected !!