Tuesday , 30 May 2023
Home Habari Mchanganyiko IGP Sirro yamemfika pomoni
Habari Mchanganyiko

IGP Sirro yamemfika pomoni

IGP Simon Sirro
Spread the love

VITA vya madaraka ndani ya Jeshi la Polisi, vimemfika pomoni mkuu wa jeshi hilo, IGP Simon Sirro. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kauli yake mbele ya maofisa waandamaizi wa jeshi hilo aliyoitoa tarehe 24 Septemba 2019, inathibitisha kuwa yupo kwenye vita pana na ya kimkakati.

Tayari taarifa za zengwe hilo anazitambua, na hata alipokuwa mbele ya maofisa hayo wakati akifungua kikao cha siku tatu cha maofisa waandamizi wa jeshi hilo na makamanda wa mikoa, kilicholenga kufanya tathmini ya miaka miwili na miezi saba ya uongozi wake amesema “tatizo ni ubinafsi…wote hatuwezi kuwa ma-IGP.”

IGP Sirro aliteuliwa kushika nafasi hiyo Mei 2017, hata hivyo kwa muda wote huo amekuwa akidaiwa kwamba hatoshi, jamboa mbalo limekuwa likimkera.

Taarifa zaidi kutoka katika jeshi hilo zinadai, baadhi ya maofisa anaowaongoza wanamzunguka, wanapeleka ‘umbea’ kutaka atemwe. Maofisa hao wanatamani leo kesho ‘wakwapue’ nafasi alionayo sasa. Hata hivyo, kulingana na taratibu inakuwa vigumu.

Kwenye kikao hicho bila kumtaja jina, IGP Sirro alionesha mvumo wa harakati hizo upande unapotokea. Kulingana na matamshi yake makali, msaidizi wake ambaye ni Kamanda Kinondoni anaingia kwenye mashaka ya harakati hizo.

“Mimi nitajuaje kama sitoshi? Kamanda Kinondoni unanipata vizuri? unanisikia? Sasa naenda mwaka wa tatu, mi nafikiri kubali yaishe tusukume sukume ifike mahala Mwenyezi Mungu akiona unatosha, atakupa.

“Sasa kwasababu wakati huu bado Mungu kasema Sirro shikilia hata kama uwezo wangu ni mdogo,” amesema IGP Sirro. Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni kwa sasa ni Mussa Taibu.

“Mara nyingi maofisa wenzangu kinachotusumbua ni ubinafsi, hakuna njia wote tukawa ma IGP hakuna. Naweza nikawa nazungumza, mwengine anaona IGP wetu hatoshi, natosha mimi sasa kama unatosha na Mungu hakukupa si ukubali sasa mimi nitafanyaje?” amehoji IGP Sirro.

IGP Sirro amesema, itakua ni aibu kwa viongozi hao endapo watalirudisha nyuma kimaendeleo jeshi hilo, badala ya kuliendeleza au kuliacha kama walivyolikuta.

“Na niwaombe sana sana maafisa wenzangu, tumepewa dhamana kubwa mavyeo makubwa. Haya mambo inabidi tuyasimamie vizuri ili jeshi tuliache kama tulivypolikuta.

“Na kama kuliendeleza tuwe tumeliendeleza jeshi kwa nafasi ambayo Mungu ametupa. Itakuwa ni aibu sana tukajikuta badala ya kuliendeleza jeshi tunarudisha jeshi nyuma,” amesema IGP Sirro.

Ameeleza, yeye hakujiteuwa mwenyewe, na kwamba muda wake ukimalizika ataondoka. Huku akieleza kwamba anamuomba Mungu wakati anaondoka aliache Jeshi la Polisi likiwa na heshima.

“Sasa vumilia, utafanyaje maanake sikujiteua mwenyewe nimekuja kuonekana wakati wako Sirro kaa hapo na itafika wakati nitaondoka. Na namuomba sana Mwenyezi Mungu niache jeshi likiwa na heshima yake. Jeshi ni kubwa ukiangalia, historia yake miaka 100 ni kubwa.

“Halafu jeshi lije liharibikie mikononi mwetu, sio kwangu tu, ukafiri jeshi likiharibika ni Sirro hapana. Historia itawarudia wote na mawazo yako ya kufikiria ningekuwa IGP, IGP ni muungano wetu wote,” amesema IGP Sirro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wenye ulemavu waiomba MISA-TAN iwajengee uwezo wa uhuru wa kujieleza

Spread the love  TAASISI ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wajawazito 2000 Korogwe washiriki Marathon, Mwenyekiti UWT amsifu Jokate

Spread the loveWANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki...

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

error: Content is protected !!