September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

IGP Sirro tuhumani

Spread the love

HATUA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kufanya mikutano ya siasa huku vyama vingine vikinyimwa uhuru huo, sasa inapigiwa yowe. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, anatuhumiwa na vyama vya upinzani kuminya uhuru wa kufanya mikutano ya kisiasa wakati chama tawala kikifanya hivyo nchi nzima.

Na kwamba, jeshi lake limekuwa likivamia mikutano ya vyama vya upinzani na kusambaratisha huku ile ya CCM ikiendelea kufanyika kinyume na tangazo la Dk. John Magufuli, Rais wa Jamhuri pia Mwenyekiti wa CCM la kusitisha mikutano hiyo.

Chama cha Wananchi (CUF), kimeungana na vyama vingine kukemea utamaduni unaojengwa wa chama tawala kufanya mikutano yake huku vyama vya upinzani vikiminywa.

Tayari Chama cha ACT-Wazalendo kimekumbana na nguvu ya jeshi la polisi katika kuzuiwa mikutano yake kama ilivyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ukimya wa jeshi hilo kukemea mikutano ya CCM, imetajwa kuwa upendeleo wa wazi kwa chama tawala huku vyama vingine vikilalamikia kuburuzwa.

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 29 Agosti 2019, Maftaha Nachuma, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanachi (CUF) – Bara amelitaka jeshi hilo kutojiingiza kwenye siasa za chama tawala na kutesa vyama vya upinzani.

Kiongozi huyo wa CUF amemkumbusha IGP Sirro kusimamia agizo la Rais Magufuli la kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa bila upendeleo.

Nachuma amesema, agizo la Rais Magufuli linatekelezwa na upande mmoja wa vyama vya wapinzani, huku viongozi wa chama tawala wakiendelea kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya kisiasa.

Kwa sasa, Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu CCM anaendelea na mikutano yake jijini Dar es Salaam ambapo baada ya kumaliza kwenye jimbo la Ubunge, linaloongozwa na Saed Kubenea (Chadema), atahamia katika jimbo la Kibamba linaloongozwa na John Mnyika (Chadema) katika kuweka mambo sawa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 24 Novemba 2019.

“IGP inabidi aliangalie hili kwani agizo la Magufuli (Rais) ni kwa vyama vyote vya siasa nchini, na siyo wao kuendelea kufanya mikutano katika maeneo yao. Lazima haki izingatiwe, kila chama kina haki zake za msingi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa,” amesema Nachuma.

Amesema, kama jeshi hilo litaendelea kuilea CCM kuendelea kufanya mikutano ya kisiasa katika maeneo mbalimbali, vyama vya upinzani navyo vitaanza kuzunguka nchi nzima.

“Leo hii tulikuwa tufanye mkutano wa chama chetu katika maeneo ya Vingunguti, jijini Dar es saalam lakini Jeshi la Polisi limetukataza na kusema kuwa, hilo ni agizo la Rais Magufuli.

“… lakini wenzetu CCM wanajiandaa tarehe 31 mwezi huu watakuwa na mkutano kule Mtwara na mageni rasmi atakuwa Mzee Pinda (Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kwanini wao wakubaliwa?” amehoji Nachuma.

Hamidu Bobali, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya chama hicho (JUVICUF), ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga amesema, hivi sasa CCM kimekuwa kikifanya mikutano yao kwa kutumia ujumbe wa Tanzania ya kijani.

Bobali amesema, mikutano hiyo ambayo CCM wamekuwa wakiifanya kwa madai ya kwenda kukagua utekelezaji wa ilani ya chama chao.

“Kama wao wanakwenda kukagua utekelezaji wa ilani, kwanini na sisi kule ambako kuna diwani wetu, mbunge wetu tusiruhusuwe kwenda kuona kuna ahadi zipi zimetekelezwa katika eneo hilo,” amesema Bobali.

Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua amesema, Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyama vingi hivyo hakuna sababu ya jeshi hilo kuendelea kukibeba chama kimoja.

“Katika mikutano hii ambayo inafanywa na watu wa CCM kwenye maeneo mbalimbali, wamekuwa wakiitumia kuwatisha wanachi kwa madai kuwa wakichagua chama kingine.

“Tunawataka hawa makatibu wa kata CCM pamoja na mabolozi, wakome kuwatisha wanachi, wawaache wachague viongozi kwa utashi wao,” amesema Sakaya.

error: Content is protected !!