August 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

IGP Sirro: Sasa washughulikieni wauaji

IGP Simon Sirro

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ameagiza polisi nchini kuwachukulia hatua watu wanaoua wenzao kwa kuwatuhumu ushirikina. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

IGP Sirro ametoa agizo wakati akizungumza na maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora leo tarehe 31 Agosti 2019, amelitaka jeshi hilo kuwafikisha mahakamani watu wanaotuhumiwa kufanya mauaji hayo.

“Bahati nzuri mlishaunda kikosi cha kupambana na haya mauaji yanayotokana na imani za kishirikina, kwa hiyo kitafanya kazi kubwa kuhakikisha hawa watu wanaohusika wanakamatwa, na si kukamatwa peke yake bali kuhakikisha kwamba wapelekwe mahakamani,” ameagiza IGP Sirro.

Aidha, IGP Sirro amewataka viongozi wa dini wa kisiasa kutoa elimu kwa jamii kuhusu suala hilo, ili waache mara moja.

“Kwenye hili suala la mauaji viongozi wa dini watusaidie sababu kukiwepo na hofu ya Mungu haya mauji yatapungua. Yamepungua lakini bado yapo,” amesema IGP Sirro.

Wakati huo huo, IGP Sirro ameagiza Jeshi la Polisi kufanya doria usiku na mchana ili kukomesha matukio ya wizi.

“Lakini matukio mengine yanayojitokeza ni uvunjaji mdogopmdogo ambao nimeelekeza doria zifanyike zaidi za usiku na mchana,” ameagiza IGP Sirro.

error: Content is protected !!