August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

IGP Sirro kutimua Polisi wabambika kesi

Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP)

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewaonya askari polisi kuacha tabia ya kuwabambikia wananchi kesi huku akiahidi kwatimua kazi watakaobainika kufanya hivyo, anaandika Mwandishi Wetu.

IGP Sirro alisema askari wa aina hiyo ndiyo anaowatafuta na kwamba akiwabaini atawatimua kazi ili kuhakikisha jeshi la polisi linaaminika katika jamii nzima.

Sirro alitoa kauli hiyo alipotoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari baada ya kumaliza shughuli zilizokuwa zimepangwa na jeshi hilo kanda maalum Tarime na Rorya.

Sirro ameonya kwamba askari wa namna hiyo hawatakiwa na kwamba kila mtumishi wa jeshi hilo lazima awe na weledi.

Amewataka wananchi watakaokumbwa na tatizo hilo kutoa taarifa kwa maofisa wa jeshi hilo ili kuwabaini wale wanaoendekeza tabia hiyo.

”Hizi habari za baadhi ya askari polisi kuendekeza tabia ya kuwabambikia kesi wananchi zinasikika mitaani, hebu wale wanye shida hiyo wawaoneni na kutoa taarifa kwa maafisa wa polisi na kamanda wa kanda maalum Tarime na Rorya ili sisi tuweze kuwashughulikia vilivyo askari polisi wa namna hiyo” alisema Sirro.

Katika hatua nyingine IGP Sirro aliwaondoa hofu waandishi wa habari kwamba watakuwa salama wanapokuwa wanafanya kazi na jeshi hilo na kuwataka kulinda maadili ya kazi yao.

error: Content is protected !!