Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko IGP Sirro awapa soma askari polisi, atangaza kiama kwa waharifu
Habari MchanganyikoTangulizi

IGP Sirro awapa soma askari polisi, atangaza kiama kwa waharifu

Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amewataka askari polisi nchini humo wasimuamini kila mtu wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi. Anaripoti Mwanaharusi Andallah, TUDARCo na Regina Mkonde, Dar ea Salaam … (endelea).

IGP Sirro ametoa wito huo leo Ijumaa, tarehe 27 Agosti 2021, akizungumza katika shughuli ya kuaga miili ya askari polisi watatu na mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya SGA, iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Polisi, Kurasini mkoani Dar es Salaam.

Askari hao walipoteza maisha Jumatano iliyopita ya tarehe 25 Agosti 2021, baada ya kushambuliwa kwa risasi maeneo mbalimbali ya miili yao ikiwemo kichwani na kijana aliyefahamika kwa jina la Hamza Mohammed, aliyedaiwa kutekeleza tukio hilo karibu na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Askari Polisi waliofariki ni, Miraji Khatib Tsingay, Emmanuel Keralya na Kangae Jackson na Mlinzi aliyefariki ni Joseph Okotya Mpondo huku kijana huyo Hamza naye akiuawa kwenye majibizano hayo ya risasi.

Akizungumzia tukio hilo, IGP Sirro amedai, wahanga wa tukio hilo walipoteza maisha kutokana na kumuamini Hamza anayedaiwa kuwashambuliwa kwa risasi.

“Lakini kwa Polisi Officers kufa kwa kupigwa risasi kichwani huwa nawaambia siku zote usicheze na mtu hovyo hovyo, usimuamini kila mtu, hii yote kwa sababu ya imani yao, walipomuona huyu mtu Hamza anawasogelea walijua mtu wa kawaida kumbe ana Pisto,” amesema IGP Sirro.

IGP Sirro amesema tukio hilo limeacha somo kwa Jeshi la Polisi, na kuwaonya watu wanaofanya uhalifu kuacha mara moja.

“Tumejifunza, ukizubaa usilaumu jeshi, ukizubaa usilaumu Serikali, askari mna mafunzo ya kutosha kwamba kuna changamoto sio kila mtu ni rafiki, sio kila mtu anapenda askari polisi na wa vyombo vya ulinzi na usalama,” amesema IGP Sirro.

Aidha, IGP Sirro amewaomba Watanzania wapaze sauti zao kulaani matukio ya namna hiyo.

“Wakati mwingine tunaambiwa tunatumia nguvu sana au hatutendi haki, lakini hapa sioni mtu akizungumzia haki ya Polisi maana yake nini, kusiwe na double standard. ku-deal na mhalifu si jambo dogo,” amesema IGP Sirro.

IGP Sirro amessma “lakini Watanzania wenzangu waelewe siku zote askari polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili ya kulinda Watanzania na ndiyo maana tumeapa kufa kwetu ni kwa risasi kwa Amiri Jeshi Mkuu wa nchi, hatuoni tabu lakini Watanzania lazima wajue na sisi tuna familia zetu.”

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Tanzania, amesema huu ni wakati kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, wanapobaini mtu mwenye mienendo isiyo faa kwa usalama wa nchi.

“Tukio la namna hili linapotokea kuna cha kujifunza, wananchi wana kitu cha kujifunza lakini wafiwa pia wana kitu cha kujifunza. Watanzania wengi ukishakuwa una mtoto mhalifu na mwizi, ukishakuwa na mtoto gaidi.

“Ukiwa na mtoto wa tabia mbaya usiposhirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama maana yake kuna mawili, la kwanza kubwa anaweza akaleta madhara kwa Watanzania lakini la pili anaweza yeye mwenyewe uhai wake ukapotea,” amesema IGP Sirro.

Amedai kama ndugu wa mtuhumiwa wa mauaji hayo wangetoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi mapema, huenda lingedhibiti tukio hilo.

“Huyu Hamza aliyoyafanyia kama ndugu zake wangewajibika vizuri, leo tusingekuwa hapa sasa,” amesema IGP Sirro.

1 Comment

  • Tupo tayari kwa lolote tutapambana na hao mbwa wenzako kwa hali na mali masilaha yamejaaa tele “mitaani” kwa hao hao askari tutawapiga na kuwapora na kuwauwa wenyewe kama alivyofanya shujaaa wetu Hamza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari Mchanganyiko

Ndege ya Precision Air yaahirisha safari kwa hitilafu, nyingine yatua kwa dharura

Spread the love  NDEGE ya Shirika la Precision Air imeshindwa kufanya safari...

error: Content is protected !!