May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

IGP Sirro awapa kibarua wenyeviti, watendaji Serikali za Mitaa

Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka wenyeviti na watendaji wa Serikali za Mitaa, kuibua vitendo vya uhalifu katika maeneo yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

IGP Sirro ametoa wito huo jana tarehe 3 Julai 2021, akizungumza na wenyeviti pamoja na watendaji wa Serikali za Mitaa, jijini Arusha.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini, amewataka viongozi hao wa mitaa kufabya doria katika vutuo na shule dini, ili kukagua masuala ya ulinzi na usalama, kwa ajili ya kudhibiti vitendo vya ugaidi.

“Miaka iliyopita moja ya matukio  nayakumbuka ilikuwa suala la ugaidi, maeneo ya Olasiti walivamia wakauwa baadhi ya waumini, ukienda MTK nako walienda wakajeruhi watu. Wanaoweza kuibua haya ni ninyi kule kwenye mitaa. Pitieni sunday school, madrasa na vyuo vya dini unaangalia. Lazima sisi viongozi tupite kujua nini kinafanyika kule ,” alisema IGP Sirro na kuongeza:

“Bila kufanya hivyo maana yake mwisho wa siku tutaingia mahala ambako hatutegemei kwenda, lakini jambo kubwa na la maana hapa ni kwamba kila mtu atimize wajibu wake. Mjue haupo pale kwa bahati mbaya, uko pale sababu sheria imetamka hivyo, Kila mtu atimize wajibu wake na moja ya wajibu wako ni suala la amani na utulivu kwenye mtaa.”

error: Content is protected !!