Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa IGP Sirro awaangukia wanasiasa  
Habari za Siasa

IGP Sirro awaangukia wanasiasa  

IGP Simon Sirro
Spread the love

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amewasihi viongozi wa vyama vya siasa na wagombea mkoani Mara, kutotumia vikundi vya vijana kufanya matukio ya uvunjifu wa amani katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

IGP Sirro ametoa wito huo jana Jumanne tarehe 13 Oktoba 2020, wakati anazungumza na wadau wa uchaguzi mkoani  humo, katika kikao kilichofanyika wilayani Musoma.

“Tusiwatumie vibaya Watanzania na wakati mwengine tunawatumia kwa kuangalia mapungufu waliyo nayo, shida walizo nazo lakini anaowatumia yeye na familia yake wanaishi vizuri sana.”

“Yule waliyemtumia sababu ya umasikini wake anapata tabu, niwaombe  sana kuhakikisha vile vikundi ambavyo tunavyo ndani ya vyama vyetu, wale vijana wanaotusapoti tukae nao na tuzungumzie suala la amani sana sana,” alisema IGP Sirro.

Aidha, IGP Sirro aliwaomba wadau wa uchaguzi mkoani Mara kutumia njia za amani kutatua migogoro ya kiuchaguzi itakayoibuka, ili mkoa huo ubadilishe historia ya kuwa na migogoro wakati wa uchaguzi.

“Ndugu zangu WanaMara, amani na utulivu wa Mara inawategemea ninyi, unatutegemea sisi. Mkoa wa Mara ukawe wa utulivu wakati wa uchaguzi, nawaomba sana suala la uvumilivu ni la msingi sana, lazima tuonyeshe mikoa mingine sisi tumebadilika.”

“Kama kuna jambo hamjakubaliana kaeni mzungumze mpate muafaka sio wa vurugu, muafaka mzuri ,” alihimiza IGP Sirro.

Wakati huo huo, IGP Sirro aliwaahidi viongozi wa kisiasa na wagombea mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu mkoani Mara, kwamba Jeshi la Polisi limebadilika na kwamba kwa sasa lina hekima hivyo kama watakutana na changamoto wazifikishe kwa ajili ya utatuzi.

“Sisi tumebadilika na tuna hekima, kama kuna jambo haliendi vizuri mtaelewana. Viongozi mkutane mzungumze mpate muafaka wa hekima wala sio muafaka wa vurugu,” amesema IGP Sirro.

Licha ya hayo, IGP Sirro alisema Jeshi la Polisi limejipanga kudhibiti vikundi vitakavyoibuka katika uchaguzi kufanya vurugu.

“Sitegemei kama kuna kikundi kitazuia MwanaMara au Mtanzania  yeyote asipige kura, uwezo huo hawana sababu kila kinachopangwa sisi tunajua, sababu Watanzania wengi hawataki vurugu wanataka amani,” alisema IGP  Sirro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!