Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko IGP Sirro atangaza operesheni kusaka wahalifu nchi nzima
Habari Mchanganyiko

IGP Sirro atangaza operesheni kusaka wahalifu nchi nzima

IGP Simon Sirro
Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro, ametangaza operesheni ya mwezi mmoja ya kusaka wahalifu nchini. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

IGP Sirro ametangaza operesheni hiyo, akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi wa Mikoa ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo Jumanne, tarehe 8 Juni 2021, jijini humo.

IGP Sirro amesema, operesheni hiyo itaanza kesho Jumatano tarehe 8 Juni 2021.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Tanzania, amewaonya watu wanaopanga kufanya uhalifu, waache mara moja, kwa kuwa jeshi hilo limejipanga kukabiliana nao kwa mujibu wa sheria.

“Kesho tunaanza operesheni ya mwezi mzima na hii operesheni ni ya nchi nzima. Jambo la msingi wale wahalifu waliotoka na kuanza uhalifu mbaya mbaya wasije kulalamika na sie tukiwafanyia mambo mabaya mabaya. Sisi tutafanya mambo mabaya kwa mujibu wa sheria,” amesema IGP Sirro.

Sirro ameongeza “suala la msingi waache uhalifu na kufanya kazi za uhalali, wakienda kinyume wasilaumu jeshi, wasilaumu Serikali.”

IGP Sirro amesema, operesheni hiyo itaenda sambamba na msako wa makosa ya usalama barabarani, ambapo ameagiza Makamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani (Traffic) wa Mikoa, kusaka magari mabovu.

“Pia , nimeelekeza operesheni ya usalama barabarani, kuna makosa ya usalama barabarani yameanza kujitokeza kama mnaona, ajali zimetokea ajali. Operesheni dhidi ya magari mabovu itaanza kesho,” amesema IGP Sirro na kuongeza:

“Nawaambia makamanda na wakuu wa Traffic mikoa yote kufanya operesheni, dhidi ya magari mabovu ambayo hayatakiwi kuwa barabarani na wahakikishe wanakua wakali kusimamia sheria za usalama barabarani.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli

Spread the loveJUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetupia lawama Serikali ikidai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!