Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko IGP Sirro asema uchunguzi sio sawa na kubeba ‘changudoa’
Habari Mchanganyiko

IGP Sirro asema uchunguzi sio sawa na kubeba ‘changudoa’

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amesema suala la kufanya uchunguzi sio sawa na kwenda barabarani na kumkuta mwanamke anayefanya biashara ya kuuza mwili ‘Changudoa’ kisha unabeba. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kamanda Sirro ameyasema hayo wakati akizungumzia kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa Mfanyabiashara Mohammed Dewji lililotokea tarehe 11 Oktoba 2018 katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.

“… sio suala unakwenda barabarani unamkuta changudoa unabeba, uchunguzi unahitaji muda na rasilimali na ndiyo maana tunapambana kutafuta wahusika,” amesema Kamanda Sirro.

Kamanda Sirro ametoa kauli hiyo kufuatia kauli za baadhi ya watu  hasa wanasiasa wa upinzani,  waliodai kwamba kamera za ulinzi ‘CCTV’ zilichezewa kwa lengo la kuvuruga uchunguzi na kuitaka serikali kuita wachunguzi wa kimataifa kuchunguza tukio hilo.

 “… sasa bahati mbaya wanasiasa ndio wapelelezi. Kila mtu anataka kuwa mpelelezi, hii kazi ni nzuri sana na huwa nasema kama ni kazi unayopenda ungeenda kuwa ofisa wa polisi.

Watu wanasema zimechezewa, wewe ndio ulikwenda ukaona hizo hazifanyi kazi? suala uchukue ninachokuambia mimi ni kwamba ile ‘footage’ haikuwa ‘clear’ kwa wakati ule, lakini baadae ukiunganisha ‘dots’ imeweza kutusaidia kujua aina ya gari,”

Kuhusu suala la kushirikiana na wachunguzi wa kimataifa, Kamanda Sirro amesema vyombo vya dola havijaona sababu za kuomba ushirikiano wa kimataifa katika kuchunguza tukio hilo kutokana kwamba viko vizuri.

Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi linashirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kufanya uchunguzi wa tukio hilo ndani na nje ya nchi ambako inasadikika gari lililotumika kumteka Mo Dewji lilitoka.

“Tumewasiliana na wenzetu wa Interpol wanafanyia kazi,  watu wetu watazunguka nchi jirani kuona tunawapata, mmiliki wa gari, dereva wa gari ambao wamejulikana na watatafutwa. Tunashirikiana vizuri na Interpol, lakini kubwa zaidi, suala la nani aje kutusaidia ni vyombo vya dola tunaweza kuona sababu hiyo na tukiona tunamshauri amiri jeshi mkuu kufanya hivyo, kwa hali tuliyo nayo sidhani kama tunahitaji msaada,” amesema Kamnda Sirro.

Hata hivyo, Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi litaendelea kufanyia kazi taarifa zinazotolewa na watu kuhusu tukio hilo, huku akitoa wito kwa jamii kutoa taarifa sahihi zitakazowezesha kupatikana kwa mfanyabisahara huyo maarufu ndani na nje ya Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!