Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari IGP Sirro amwonya Lissu, amtaka kuripoti Polisi
Habari

IGP Sirro amwonya Lissu, amtaka kuripoti Polisi

Spread the love

INSPEKTA Jenerali wa Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro amemtaka Tundu Lissu, mgombea urais wa nchi hiyo kupitia Chadema katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 kuripoti Kituo cha Polisi Moshi Mkoa wa Kilimanjaro. Anaripoti Mwandiushi Wetu…(endelea)

Pia, ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaotaka kuvuruga uchaguzi huo akisema “itafika mahali tutawashughulikia sana kwa mujibu wa sharia.”

IGP Sirro akizungumza leo Alhamisi tarehe 1 Oktoba 2020 amesema, Lissu amekuwa na tabia ya kukaripia na kugombeza askari polisi na jana amefanya hivyo akiwa Kilimanjaro kwenye mikutano yake ya kampeni na tayari amezungumza na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema kuhusu hilo.

“Viongozi wa Chadema, wamekuwa na tabia ya kukaripia, kugombeza askari polisi na tumeona mara kadhaa Tundu Lissu anagombana polisi na jana nimeongea na kiongozi wake, Mbowe akae na watu wake wazungumze utii wa sheria bila shuruti.”

“Anayoyafanya Watanzania wenye hekima wanayaona, anayoyafanya Watanzania wenye hekima na wazalendo wa nchi hii wanayaona, Lissu hayuko juu ya sheria, polisi tukiamua kutimiza wajibu wetu asilalamike na chama chake,” amesema IGP Sirro

Amesema, vyama vya siasa viko karibu 12 na jeshi la polisi limepewa wajibu wa kulinda watu na mali zake ndani ya nchi na Lissu hana uwezo wowote wa kupambana na jeshi la polisi.

“…aende aripoti kituo cha polisi Kilimanjaro ili aeleze hayo aliyoyafanya jana,” amesema IGP Sirro.

“Niwaombe wagombea wote, suala la udiwani, ubunge na urais bila amani na utulivu hauwezi kufanya siasa, tuheshimu sheria zilizopo na inaonekana kuna viongozi wachache wanataka fujo ifanyike ili uchaguzi usifanyike, hiyo nafasi hawana, uchaguzi utafanyika lakini itafika mahali tutawashughulikia sana kwa mujibu wa sharia,” amesema IGP Sirro

Kwa mujibu wa ratiba ya kampeni iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaonyesha kuanzia leo hadi 3 Oktoba 2020, Lissu hana mkutano wowote wa kampeni na leo alikuwa njiani kutoka Moshi, Kilimanjaro kwenda Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!