July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

IGP Sirro ampa neno bosi mpya Takukuru, yeye atoa neno

Spread the love

 

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro, amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kamishna, Salum Hamduni, kuliwakilisha vizuri Jeshi la Polisi, katika utekelezaji wa majukumu yake mapya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar Es Salaam … (endelea).

Sirro ametoa neno hilo leo Jumatatu, tarehe 17 Mei 2021, jijini Dar es Salaam, baada ya kumvalisha cheo cha Kamishna wa Polisi, Hamduni, kwa niaba ya Rais wa Tanzania, Samia Suhulu Hassan.

Tarehe 15 Mei 2021, Rais Samia, alimteua Hamduni, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), kuwa mkurugenzi mkuu wa Takukuru, kuchukua nafasi ya Brigedia John Mbungo ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Pia, Rais Samia, alimpandisha cheo, Hamduni kutoka naibu kamisha kuwa kamisha.

Akizungumzia uteuzi huo, IGP Sirro amesema “naamini huwa una angalia kwenye mitandao, unajua siku hizi lazima uangalie kwenye mitandao inasema nini teuzi zikifanyika, nimeangalia kwenye mitandao una full sapoti ya Watanzania.”

“Kuonesha kwamba umetoka polisi na polisi ni idara ya upelelezi, naamini utapeleleza vizuri na mwisho wa siku utawatendea haki Watanzania,” amesema IGP Sirro.

Amemshauri Hamduni, kutii kiapo chake, kwa kuhakikisha anawatendea haki Watanzania.

“Siku zote kazi yetu kubwa kuhakikisha kiapo ambacho umeapa mbele ya maofisa na mbele yangu, unatimiza kile kiapo chako, kama unavyoona nimekukabidhi Katiba na Police General Order ambayo ndio muongozo wa kazi zetu za kila siku,” amesema IGP Sirro na kuongeza:

“Sisi tunasimamia sheria lakini kikubwa zaidi kuhakikisha sisi sio wa kwanza kuvunja sheria, mimi sina mashaka na hilo. Utendaji wako naamini unakwenda kutuwakilisha vizuri, naamini utakwenda kuwatendea haki Watanzania.”

Kwa upande wake, Hamduni amesema, katika majukumu yake mapya atahakikisha haki inatendeka ndani ya nchi.

“Imani kubwa ya Jeshi na imeniwezesha pengine kuonekana nafaa kuweza kuhudumu maeneo mengine, yote msingi wake kuhakikisha tunawahudumia Watanzania katika kulinda maisha yao na mali zao na kuhakikisha kwamaba haki ndani ya nchii inatendeka,” amesema CP Hamduni.

error: Content is protected !!