March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

IGP  Sirro aambiwa aanze na Makonda

Spread the love

Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amemtuhumu  kamanda Simon Sirro, mkuu wa jeshi la polisi nchini kuwa jeshi lake linawafahamu  watu ambao inadai hawajulikani, anaandika Hellen Sisya.

Kigaila ameyasema hayo leo hii katika mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

Aidha, amesema jeshi la polisi linatakiwa kuanza na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambaye anadaiwa kuvamia kituo cha Clouds akiwa ameambatana na vijana wenye silaha.

Kigaila amehoji kitendo cha jeshi hilo kutaka kupelekewa taarifa rasmi ili liweze kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio la shambulio la risasi dhidi ya Tundu Lissu.

error: Content is protected !!