Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko IGP apangua makamanda wa mikoa, Muslim apelekwa Makao Makuu
Habari Mchanganyiko

IGP apangua makamanda wa mikoa, Muslim apelekwa Makao Makuu

IGP, Camilius Wambura
Spread the love

 

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, amefanya mabadiliko madogo ya Makamnda wa Polisi wa Mikoa ambapo wengine wamehamishiwa makao makuu na wengine kuhamishwa mikoa mingine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mabadiliko hayo yamemgusa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mororgoro, SACP Fortunatus Muslim ambaye amehamishiwa kitengo cha mipango makao makuu wa polisi Dododma na nafasi yake kuchukuiwa na ACP Alex Mukama ambaye alikuwa Kmanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

Pia IGP Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

Aidha amemhamisha ACP Shadrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Kamada wa Polisi Mkoa wa Rukwa.

Taarifa ya mabadiliko hayo imetolewa leo Ijumaa tarehe 6 Januari, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!