Friday , 9 June 2023
Home Kitengo Michezo IFAB yafanya mabadiliko ya kanuni kwenye Soka
Michezo

IFAB yafanya mabadiliko ya kanuni kwenye Soka

Mpira wa miguu
Spread the love

BODI ya Kimataifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (IFAB) imefanya mabadiliko ya kanuni ya mchezo wa soka kwenye kikao kilichofanyika wiki iliyopita nchini Scotland na mabadiliko hayo yataanza kutumika misimu ujao wa mashindano 2019/20. Inalipoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

IFAB imefanya jumla ya mabadiliko saba yakihusisha sehemu ya ndani ya uwanja na nje ya uwanja wakati mchezo husika ukiendelea.

Badiliko la kwanza ni kutokuwa na mrejesho (rebound) kwenye pigo la penalti na mchezo utasimama kwa kuanzishwa kama mpira wa penalti utakuwa umeokolewa au kugonga mwamba kwa hiyo hakutokuwa na haja ya wachezaji kujipanga nje ya boksi wakati penalti hiyo ikipigwa.

Badiliko la pili, endapo goli lolote litafungwa likiwa limegusa mkono wa mchezaji kwa makusudi au bahati mbaya halitakubalika na endapo mchezaji atakuwa anafanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja ili kuepusha swala la kupoteza muda.

Mabadiliko mengine yaliofanywa na bodi hiyo ni mpira wa kuanza kwa kipa (goal kick) mchezaji ataruhusiwa kuugusa mpira huo hata akiwa ndani ya eneo la boksi kutoka kwa kipa tofauti na hapo awali mchezaji alikuwa haruhusiwi kugusa mpira huo mpaka utoke nje ya boksi.

Kwa upande wa makocha nao watakuwa wanaoneshwa kadi ya njano na nyekundu tofauti na sasa wanaambiwa watoke tu kwenye eneo la benchi la ufundi na baada ya kuoneshewa kadi hiyo nao watakuwa wanakosa baadhi ya michezo.

Maeneo mengine yaliofanyiwa mabadiliko ni kwenye kuweka ukuta wa kuzuia mpira wa adhabu ndogo (foul) ambapo wachezaji wa wanapiga mpira huo hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mpira huo, na kwenye adhabu kubwa ya penalti makipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja kwenye mstari na mwingine kuamua ukae popote.

Hivi karibuni mchezo wa mpira wa miguu umekuwa ukifanyiwa mabadiliko mengi ikiwamo ya teknolojia kama kutumia video katika maamuzi (video assistance referee) iliyotumika kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika Urusi Juni, 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Yanga waitwa Ikulu kesho Jumatatu

Spread the love RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu, tarehe...

error: Content is protected !!