April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Idd Simba afariki dunia

Marehemu Idd Simba, enzi wa uhai wake

Spread the love

MFANYABIASHARA, Mbunge wa zamani wa Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idd Simba (85) amefariki dunia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya familia yake zinaeleza, Simba amefariki leo tarehe 13 Februari 2011, wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Taarifa za kifo cha Simba ambaye alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya Tatu, chini ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, zimedhibitishwa na mtoto wake Sauda Simba Kilumanga.

Sauda ameeleza kwamba, taratibu za msiba huo bado hazijapangwa, na kwamba utaratibu utaeleza hapo baadaye.

error: Content is protected !!