January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Idd Azzan amfikisha Mtulia Mahakamani

Spread the love

USHINDI wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia mbunge wake, Maulidi Mtulia unapingwa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Idd Azzan ambaye alikuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndiye aliyefungua kesi hiyo katika Mahakama  Kuu Kanda ya Dar es Salaam tarehe 25 Novemba mwaka huu. Anaiomba mahakama hiyo itengue ushindi wa Mtulia.

Miongoni mwa madai ya Azzan kwenye mahakama hiyo ni pamoja na kuwepo kwa vituo hewa vya kupigia kura, mawakala wake walitolewa nje katika chumba cha kuhesabia kura na kwamba hawakushuhudia uhesabuji wa kura, watu waliingia na kura feki ndani ya vituo.

Lakini pia Azzan amedai wasimamizi wa vituo vya kupigia kura walitumia nakala za matokeo ya wakala wa Mtulia kujumlisha na kutoa matokeo, kutofautiana kwa kura zilizopo kwenye nakala za mawakala wa Mtulia na zile zilizobandikwa ubaoni, jina la Mtulia lilikuwa limeondolewa katika majina ya wagombea ubunge kwenye Jimbo la Kinondoni na kwamba, ushindi wake ni batili.

Akizungumza na MwanaHalisionline leo Mtulia amesema, ameyapokea madai hayo na kwamba yupo tayari kupambana nayo kwani anaimani mahakama itatenda haki kulingana na matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

“Nimeshangazwa na hatua hiyo japo nilijua tu kama atafanya hivyo kwani Azzan ni mtu ambaye hataki kukubaliana na maamuzi ya wananchi japo kuwa anajua kuwa ameshindwa.

“Siku hizi kwenda mahakamani kupinga matokeo kwa CCM imekuwa kama fasheni. Tatizo Azzan alijipa moyo kuwa Jimbo la Kinondoni ni lake hawezi kupingwa ndio maana alipandisha presha siku ya kutangaza matokeo,” amesema Mtulia

Mbali na hilo, Mtulia amesema kwa sasa hana presha na kesi hiyo inayomkabili kwa kuwa anauhakika na ushindi, bali anajipanga na mwakani atakaporudi bungeni afanye jitiada za kuwatafuta wafadhili mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia wananchi wake.

Aidha, katika uchaguzi uliopita, Mtulia alitangazwa kushinda kwa kupata kura 70,337 dhidi ya Azzan ambaye alitangazwa kupata kura 65,966.

error: Content is protected !!