July 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Idadi ya wanaojiua Marekani yaongezeka

Spread the love

KITUO cha Afya nchini Marekani kimeeleza kuwa, takwimu ya watu wanaojiua katika taifa hilo imeongezeka kwa asilimia 25 katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, anaandika Wolfram Mwalongo.

Idadi hiyo inatajwa kuwa kubwa kuwahi kutokea nchini humo tangu mwaka 1980 ambapo utafiti huo umefanywa kwa watu warika zote huku wanawake watu wazima idadi yao imenaonekana kuwa juu kwa asilimia 36.

Vifo vya wasichana wa umri wa kati ya miaka 10 na 14 vimeongezeka mara tatu zaidi katika kipindi hicho huku wataalmu wakisema, huenda vitendo hivyo vinachangiwa na mitandao ya kijamii.

Profesa Robert D Putnam, Chuo Kikuu cha Harvard amesema, uhusiano baina ya umaskini na hali ya afya pia huenda ikawa ni visababishi.

error: Content is protected !!