March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Idadi wanafunzi waliopewa ujauzito na madereva bodaboda utata

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa ni vigumu kupata idadi ya wanafunzi waliopewa mimba ba madereva wa pikipiki maafuru kwa madereva wa bodaboda. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Kutokana na hali hiyo serikali imeeleza kuwa takwimu za wanafunzi waliopata mimba hazikokotolewi kwa kuainisha makundi ya wanaume waliowapa ujauzito wanafunzi hao.

Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi Teknologia, William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Toufiq (CCM).

Katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuthibiti hali ya madereva bodaboda wanaowaadaa baadhi ya wanafunzi wa kike.

Aidha alitaka kujua ni wanafunzi wangapi wanaoripotiwa kupewa mimba na bodaboda katika kipindi cha miaka 3 iliyopita.

Akijibu swali hilo, Ole Nasha, amesema kuwa serikali inatambua kuwa wapo wanaume wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji, ulawiti na kuwapa mimba baadhi ya wanafunzi.

Amesema kuwa baadhi ya madereva bodaboda wameripotiwa kujihusisha na vitendo hivyo viovu.

Amesema vitendo hivyo utokana na tabia mbaya, Vishawishi na changamoto za mazingira kama vile umbli kutoka nyumbani kwenda shuleni.

error: Content is protected !!