MAHAKAMA ya Kimataifa ya Uhalifu wa kivita (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin. Vinaripoti Vyombo vya Habari vya Kimataifa …(endelea).
ICC inadai kuwa kiongozi huyo anahusika na uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha watoto kutoka Ukraine kwenda Urusi kinyume cha sheria.
Inasema uhalifu huo ulifanyika nchini Ukraine kuanzia tarehe 24 Februari 2022 – wakati Urusi ilipoanzisha uvamizi wake kamili.
Moscow imekanusha madai ya uhalifu wa kivita wakati wa uvamizi huo.
Mahakama ya ICC imemshtaki Putin kwa kuhusika katika kuwafukuza watoto, na inasema ina sababu za kuridhisha kuamini kuwa alifanya vitendo hivyo moja kwa moja, pamoja na kufanya kazi na wengine.
Aidha, Mahakama pia ilisema kiongozi huyo wa Urusi alishindwa kutekeleza haki yake kuwazuia wengine waliowahamisha watoto.
Kamishna wa haki za watoto wa Urusi, Maria Alekseevna Lvova-Belova, pia anasakwa na mahakama hiyo.
Hata hivyo, kibali hicho cha kumkamata putin na Bi Lvova-Belova kutolewa, ICC haina mamlaka ya kuwakamata washukiwa, na inaweza tu kutumia mamlaka ndani ya nchi ambazo zimesaini makubaliano yaliyounda mahakama hiyo.
Urusi sio mwanachama wa makubaliano hayo – kwa hivyo hakuna uwezekano wa kiongozi huyo kuwasilishwa mbele ya mahakama.
Leave a comment