May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

#LIVE: Rais Magufuli awasili Lupaso kumzika Mkapa

Spread the love

Dk. Shein afikisha salamu za Wazanzibari kwa Mkapa

Saa 7:46 mchana

DAKTARI Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Zanzibar amemtaja Hayati Benjamin Mkapa kwamba aliyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar.

Akitoa salamu za Wazanzibari wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa kwenye msiba wa Mzee Mkapa, Lupaso mkoani Mtwara leo Jumatano, Dk. Shein amesema, Zanzibar inamuheshimu Mzee Mkapa kwa mapenzi yake na visiwa hivyo.

“Nimesimama kutoa salamu zangu na kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar za msiba mkubwa uliotupata Watanzania, Nawapa salamu zangu na Serikali ya Zanzibar.”

“Mkapa aliyatunza Mapinduzi ya Zanzibar kwa vitendo, tunamuheshimu kwa hali na uzalendo wake huo. Jukumu letu ni kumuombea mzee wetu kwamba Mungu amsamehe makosa yake,” amesema Dk. Shein.

Rais Magufuli awasili Lupaso kumzika Mkapa

 Saa 7:28 mchana

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewasilia nyumbani kwa Hayati Rais mstaafu awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa Lupaso wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara kuhudhuria mazishi ya Mkapa yanayofanyika leo Jumatano.

Mara baada ya kuwasilia nyumbani hapo, Rais Magufuli aliwasalimia viongozi mbalimbali waliohudhuria shughuli hiyo wakiwemo Marais wastaafu wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Ali Hassan Mwinyi.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

 

Mamia Lupaso wapata fursa kumuaga Mkapa

Saa 4:50

Mamia ya wakazi wa Kijiji cha Lupaso, Mtwara wamepata fursa ya kumuaga Hayati Benjamin Mkapa leo Jumatano tarehe 29 Julai 2020.

Kwa mujibu wa ratiba, Hayati Mkapa aliyefariki tarehe 23 Julai 2020, jijini Dar es Salaam saa 3: 30 usiku kwa mshtuko wa moyo na atazikwa baadaye kijijini.

Tayari misa imekamilika iliyoongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Gervas Nyaisonga.

Katika misa hiyo, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Tanzania.

Wengine waliohudhuria misa hiyo ni, Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Mrisho Kikwete.

Pia, vingozi wa dini, mawaziri, wakuu wa tasisi, wanasiasa wameshiriki kuuaga mwili wa Mkapa.

Vatcan yatuma salamu msiba wa Mkapa

Saa 3:48

Mkao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani Vatcan nchini Italia, wametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, amewaeleza waombolezaji waliokusanyika kwenye ibada ya mwisho ya kumuaga Hayati Benjamin Mkapa aliyefariki dunia tarehe 23 Julai 2020, jijini Dar es Salaam.

Amesema, kwa muda mrefu Vatcan imekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania na kwamba, kutokana na uhusiano huo mzuri, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi aliwahi kumualika nchini Papa John Paulo wa II.

Ibada ya mwisho ya Mkapa Lupaso

Saa 3:00

MAMIA ya wakazi wa Lupaso, Masasi mkoani Mtwara, wamejumuika na familia ya Mkapa kwenye ibada ya mwisho ya Hayati Benjamin Mkapa inayofanyika leo tarehe 29 Julai 2020.

Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na wa vyama vya siasa. Miongoni mwao ni Rais wa Tanzania John Magufuli; Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi; Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.

Wengine ni Mama Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Tanzania; Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu; Balozi Seif Ali Idd, Makamu wa Rais Zanzibar na Joseph Wariob, Jaji Mkuu Mstaafu.

Maombi na nyimbo za kuabudu zinaendelea kwenye viunga hivyo. Hayati Mkapa alifariki tarehe 23 Julai 2020 na anatarajiwa kuzikwa leo kijijini humo.

error: Content is protected !!