Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Ibada ya kumuombea Hayati Magufuli yafanyika Chato
Habari Mchanganyiko

Ibada ya kumuombea Hayati Magufuli yafanyika Chato

Spread the love

 

IBADA maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli, imefanyika katika Kanisa la Mt. Yohana Mria Muzeyi, Parokia ya Mlimani, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, ikiwa ni maadhimisho ya miaka miwili tangu kifo chake kilichotokea tarehe 17 Machi 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Ibada hiyo imefanyika leo tarehe 17 Machi 2023, kanisani hapo na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi, ambapo familia ya Hayati Magufuli, ikiongozwa na mjane wake, Mama Janeth Magufuli, ilishiriki.

Mbali na familia ya Hayati Magufuli, viongozi wa Serikali walioshiriki ibada hiyo ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Zanzibar, upande wa vijana, Mwanaenzi Suluhu Hassan.

Hayati Magufuli alifariki dunia akiwa madarakani, katika Hospitali ya Mzena , Makumbusho jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya maradhi ya moyo.

Kufuatia kifo chake, aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa Rais.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!