Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Hyundai yatambulisha gari toleo jipya la Tucson
Habari Mchanganyiko

Hyundai yatambulisha gari toleo jipya la Tucson

Muenokano wa Gari ya Tucson toleo jipya la 2017
Spread the love

KAMPUNI ya Hyundai East Afrika LTD imezindua magari yake mapya ya kisasa aina ya Tucson toleo la mwaka 2017 katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), anaandika Hamisi Mguta.

Tucson hiyo mpya ina muonekano mzuri wa kuvutia nje na ndani huku ikiwa imetengenzwa kwa ufanisi wa hali ya juu ambapo kiwango cha uchumi wa mafuta kimeongezwa zaidi ya matoleo ya Hyundai yaliyopita.

“Gari hii mpya ya Tucson imesheheni kile ambacho wateja wetu wanatafuta katika kusaka ushindani wa bei wa kila ngazi, amesema Mehboob Karmali, Mkurugenzi Mtendaji wa Hyundai East Africa LTD.

“Magari ya Hyundai hujulikana kwa mtindo wake safi na mafanikio ya juu, uaminifu wa katika madaraja mbalimbali ya ubora duniani, lengo letu kujitolea kwa bidhaa zetu ni kufanya mambo vizuri. Tunakwenda kuwafurahisha wateja wetu kwa kutoa gari mpya ya kisasa ambayo hawawezi kusahau kwakuwa tunataka kuendelea Kuongoza katika soko na sekta hiyo na kuwafanya wamiliki gari za Hyundai kuwa na faraja,” aliongeza Karmal.

Vipimo vya gari aina ya Tucson

Zaidi ya hayo, Tucson imetengenezwa kwa uendeshaji wa automatic ambayo ina upeo wa usalama wa hali ya juu.

Teknolojia za usalama kama vile breki ya automatiki pindi inapotokea dharura na mfumo wa onyo wa kuondoka.

Mawasiliano ya kiautomatiki ya kuokoa usalama na kamera ya nyuma pia itatolewa.

Hata hivyo kampuni hiyo imetoa gari ya wagonjwa aina ya H-1 ambayo imewekwa kitanda ambacho kina mfumo wa kiautomatiki katika ufungukaji huku visimamio vyake ufunguka vyenyewe.

Antony Nyeupe, Mtendaji mkuu wa mauzo katika Kampuni hiyo amesema gari hiyo ya kubebea wagonjwa ni ya kisasa zaidi na kuwa kampuni hiyo ipo tayari kufanya kazi na mashirika mbalimbali watakayohitaji kununua gari hiyo.

Anthony Nyeupe, Mtendaji mkuu wa mauzo akivuta kitanda cha kubebea mgonjwa kichopo ndani ya gari hiyo aina ya H-1

 

Vipimo vya Gari aina ya H-1

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!