Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Michezo Huwezi kujua kesho ya mpinzani wako
MichezoTangulizi

Huwezi kujua kesho ya mpinzani wako

Spread the love

SITAKI kumtetea Patrick Aussems na wala sitaki kusimama upande wa Masoud Djuma lakini najisikia kusema jambo dogo tu baada ya dakika 90 pale CCM Kirumba. Anaandika Mchambuzi Maalum … (endelea).

Ghafla tu timu inabadilisha kocha mkuu, ndio kubadilisha kocha si dhambi hakuna kitu chochote kinaweza kuzuia andiko hilo muda wowote tu unaweza kubadilisha kocha.

Wakati anakuja kocha mpya tayari timu anaikuta mikononi mwa kocha msaidizi kocha msaidizi anajua kila kitu kuhusu wachezaji wake kwa sababu amekaa nao muda mrefu kabla ya kocha mwingine kuja unadhani nasimama upande wa Masoud au Patrick?

Timu inapata droo dhidi ya Ndanda sawa ni matokeo ya mpira baadae timu inakwenda kupoteza mchezo dhidi ya Mbao sawa yote ni matokeo ya mpira kwa sababu mpira ni sayansi kubwa sana kuizidi ile ya Mark Zuckerberg uliwahi kujiuliza kwanini timu huwa zinakuwa na makocha wasaidizi? uliwahi kujiuliza kazi ya kocha msaidizi ni nini?

Nataka kucheka lakini naogopa utasikia amebaki Dar kuwanoa Haruna Niyonzima na Juuko Murshid pamoja na wengine  hapo ndiyo huwa najisikia kucheka kabisa lakini utaonekana mchawi mbele ya watu wenye uchungu na Simba yao

Kocha msaidizi anaijua vyema Chemistry ya timu yake kuanzia golini hadi kwa winga wa kushoto, kocha msaidizi anajua vyema nani acheze na nani katika eneo la kiungo kutengeneza uwiano mzuri wakuleta mashambulizi yenye nguvu.

Siku moja babu yangu wakifaransa alipewa kazi yakuinoa Simba akaikuta chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma ambae alipokea mikoba kwa Joseph Omong namzungumzia Pierre Lechantre

Akaikuta timu inacheza 3:5:2 unafikiri alivunja huo mfumo? hapana timu ilicheza mfumo huo huo mpaka alivyoipa tena mkono wa kwaheri baada ya miezi sita tu kumalizika nahisi kuna tatizo tena tatizo kubwa.

Yule mzungu mwingine nilimsikia vyema akiongea radio fulani sina uhakika kama alikuwa sahihi au hakuwa sahihi kuhusu swala hili hili la makocha kama kunatofauti zingemalizwa tu.

Mafanikio ya timu huja baada ya maelewano mazuri kati ya kocha mkuu na kocha msaidizi sina uhakika kama kuna tatizo kati ya kocha mkuu na kocha msaidizi lakini nafikiri kuna mgogoro nani alikwambia ukiwa na migogoro timu inaweza kufanya vizuri? unajikuta unatengeneza makundi ndani ya timu jambo ambalo si zuri.

Nimeona vyema mechi dhidi ya Mbao timu imecheza vyema lakini imetengeneza nafasi ambazo hawakuzitumia. Lakini navyoitazama Simba nahisi kuna tatizo hasa yule jamaa wakati umepaniki anatoka Shiza Kichuya anaingia kinda Rashid Juma aisee.

Na niwapongeze tu Mbao maana hakuna jambo gumu kama kushinda mbele ya Simba ni jambo gumu lakini wameweza ijayo mechi dhidi ya Mwadui… habari za Mwadui anazo Razack Abalora..

Hivi Msimu huu Simba si anacheza Ligu ya Mabingwa Afrika? Lazima kama kuna tofauti zimalizwe haraka sana unafungwa na Mbao wakati unatakiwa kujiandaa kucheza dhidi ya TP Mazembe au Al Masry.

Nataka kuendelea kuandika lakini najikuta nataka kuishia hapo mikono inatetemeka mno misri ya mgonjwa mbele ya daktari wa meno tatizo nchi yangu huwa haipendi ukweli kabisa.

Lakini ligi bado na ndio kwanza inaanza huwezi kuijua kesho ya mpinzani wako, ngoja niendelee kutazama tu muda utaongea ebu tujifunze kwa matokeo ya hizi mechi mbili alafu tuzungumze lugha moja ili Simba ianze kufanya vema.

Makala hii imeandikwa na kuwekwa kwenye mitandao ya kijamii na mchangiaji/mchambuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za SiasaTangulizi

Mkataba wa Tanesco, Songas watakiwa bungeni

Spread the loveWAKATI mkataba wa Ununuzi wa Umeme kati ya Shirika la...

Michezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Michezo

Unamalizaje Jumapili hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Jipigie pesa na Meridianbet leo hii

Spread the love KAMPUNI kubwa ya ubashiri Tanzania inakwambia hivi huu ndio...

error: Content is protected !!