Wednesday , 27 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Huu ni unyama; Waziri ahuzunika mateso ya mama, kichanga chake
Habari Mchanganyiko

Huu ni unyama; Waziri ahuzunika mateso ya mama, kichanga chake

Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni
Spread the love

UNYAMA na vitendo vya ukiukwaji wa sheria vimelalamikiwa na Mhandisi Hamad Massauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waziri Massauni ameeleza kukithiri kwa vitendo hivyo mahabusu, huku akitolea mfano kisa cha mwanamke na mtoto wake wa mwaka mmoja na nusu, waliosota mahabusu kwa mwaka mmoja na nusu.

Ameeleza kisa hicho wakati akizungumza na vyombo vya habari,  kuhusu ziara yake aliyoifanya ya kutembelea mahabusu ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.

Akieleza kisa hicho amesema, mwanamama huyo na kichanga chake, waliwekwa mahabusu, akituhumiwa kuiba kitenge chenye thamani ya Sh. 30,000.

Mhandisi Massauni ameeleza kuwa, kilichosababisha changamoto hiyo ni mamlaka husika kutowajibika ipasavyo, huku akiinyooshea kidole Kamati za Kuharakisha kesi nchini.

“Kwa sababu ya kutowajibika kwetu ipasavyo, naomba nitoe mfano mmoja, nilimkuta msichana mmoja ana mtoto mdogo wa mwaka mmoja na nusu yuko zaidi ya miezi mitano katika mahabusu, lakini hajawahi kupelekwa mahakamani. Na uhakika angepelekwa mahakamani, siku ya kwanza tu hakimu angempa dhamana, “ amesema Mhandisi Massauni na kuongeza.

“Kosa mume wake alikuja na kitenge nyumbani kwake yeye akavaa akakamatwa,  akaambiwa ameiba kitenge cha 30,000. Mtu kama huyu mnamuweka gerezani miezi mitano hadi sita, halafu hakuna mtu anayeguswa kwa hili jambo kuchukua hatua za haraka.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari Mchanganyiko

Wizara ya madini kurusha ndege ya utafiti wa madini Geita

Spread the loveKutokana na mchango wa wachimbaji wadogo wa madini kwenye pato...

Habari Mchanganyiko

Jafo aagiza kampuni za madini kuzingatia utunzaji mazingira, azitaka zijifunze kwa GGML

Spread the loveWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

error: Content is protected !!