Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Utetezi wa Kubenea, Komu Chadema huu hapa
Habari za SiasaTangulizi

Utetezi wa Kubenea, Komu Chadema huu hapa

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea pamoja na wa Moshi Vijijini, Anthony Komu wametoa ufafanuzi wao kuhusu sauti iliyosambaa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni, wakijadili kuhusu ruzuku ya chama hicho na uhusiano wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kubenea na Komu mbele ya mkutano wao na wanahabari uliofanyika leo tarehe 18 Oktoba 2018, wamejitetea kuwa, haikuwa dhamira yao kuona kwamba mazungumzo hayo yaliyoleta taswira mbaya kwa Chadema, yanasambaa kwa umma kupitia mitandao ya kijamii, bali isivyo bahati sauti hiyo ilivuja.

Wamejitetea kuwa, dhamira ya mazungumzo yao kuhusu suala la ruzuku ya chama hicho na ukaribu wa Mbowe na Jacob, ni kutaka kuona kwamba malalamiko juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya ruzuku za Chadema yanayotolewa na baadhi ya watu, yanafanyiwa kazi.

Wameeleza kuwa “Hapa kuna mkaguzi wa ndani ambaye anakagua hesabu za chama, kama kuna mtu anafahamu kuna tatizo la fedha, hizi pesa ni za umma na unapaswa kuchukua hatua, hata hayo tuliyokuwa tunazungumza ni katika msingi huo huo, kama kuna mambo hayaendi vizuri, viongozi wetu wanatukanwa tukanwa,hayo ndiyo yangefanyiwa kazi, na hiyo ndio ilikuwa hoja yetu.”

Komu ameeleza kuwa, kilichopelekea mazungumzo hayo, ni hoja kuhusu matumizi ya ruzuku ya Chadema waliyokutana nayo kwenye mazungumzo ambayo hakuyataja chanzo chake, na kupelekea yeye na Kubenea kuanza kuzungumzia hoja hiyo katika mazungumzo yao ya faragha.

“Ni kwamba klipu ilitoka bahati mbaya na mazungumzo yake hayakutoka eneo lolote,ukisikiliza maelezo mengine yote yangekuwa yamerokodiwa hakukuwa na dhamira ya kumdhuru mtu, ni hoja tuliyokutana nayo kwenye mazungumzo fulani, ikatufanya tuzungumze yale mambo,” amesema Komu.

Kuhusu tuhuma za kutaka kumdhuru Meya Jacob, wabunge hao wamejitetea kuwa, hawakuwa na dhamira ya kumdhuru meya huyo.

“Kudhuru ni jinai, na kama ni jinai haikupaswa kuishia kwenye Kamati Kuu, ni kweli ilikuwa klipu yetu lakini kusema nitamtoa mtu fulani ina tafsiri nyingi, kumtoa sadaka au kumtoa mtu nje. Hatukuwa tumelewa bali tulikuwa tunajadiliana kuhusu Mada tuliyoikuta huko nje,” amesema Komu.

Naye Kubenea amejitetea kuwa “ Hatuna mgogoro na Jacob tunashirikiana nae, tunafanya kazi vizuri na ushahidi wa hilo kama tuko pamoja hata juzi kwenye uchaguzi wa naibu meya wa jiji , CCM walitaka kuweka kura kwapani lakini tuliungana kwa pamoja kuzuia hilo. Na hata katika Halmsahauri ya Ubungo tunashirikiana vizuri.”

Komu na Kubenea wamemuomba radhi Mbowe na Meya Jacob pamoja na watanzania kutokana na sakata hilo na kuahidi kuahidi kutekeleza maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema waliyopewa baada ya kuwahoji hapo jana.

“Chama ni kikubwa kuliko sisi, na baada ya kamati kuu kukutana, wakatoa mazimio na sisi kwa kutambua kama viongozi wa chama hayo maazimio tutayasikiliza, tushawasilisha barua kwa saa zile tulizotakiwa kuwasilisha na kuomba msamaha, na sasa tunachukua nafasi ya pili ya kuomba radhi kwa chama na wanachama wenyewe na watanzania wote wanaotaka kuona tunaendelea na ustawi wa chama, na kwa wale waliotajwa katika mazungumzo ya faragha na kutokana na teknolojia ikanishinda, ikasababisha ajali, ninawaomba radhi,” amesema Komu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!