Tuesday , 23 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Huu hapa uamuzi wa Mahakama juu ya masuala tisa ya kupinga ushindi wa Ruto
KimataifaTangulizi

Huu hapa uamuzi wa Mahakama juu ya masuala tisa ya kupinga ushindi wa Ruto

Spread the love

 

MAJAJI saba wa Mahakama ya Juu nchini Kenya wametoa uamuzi wa pamoja wa kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wa Rais Mteule William Ruto kwa kile walichoeleza ni kukosekana kwa ushahidi wenye mashiko juu ya masuala tisa yaliyokuwa yanataka uamuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Uamuzi huo umesomwa leo Jumatatu tarehe 5, Septemba, 2022, na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu nchini humo, Martha Koome baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano tarehe 31, Agosti, 2022.

Katika uamuzi huo Mahakama, kwa maoni yake iliyozingatiwa, haikupata ushahidi wa udukuzi na kwamba hakuna ushahidi uliotolewa kuonyesha kuwa mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati na wafanyikazi wengine wa IEBC walihusika.

Hivi ndivyo mahakama ilivyoamua:

Teknolojia iliyotumwa na IEBC kwa uendeshaji wa uchaguzi mkuu wa 2022 iliafiki viwango vya uadilifu, uthibitisho, usalama na uwazi ili kuhakikisha matokeo sahihi na yanayoweza kuthibitishwa. (Kwa kauli moja. Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Mohammed K Ibrahim, Njoki Ndung’u, Dkt Smokin Wanjala, Isaac Lenaola, William Ouko).

Hakukuwa na kuingiliwa kwa upakiaji na usambazaji wa Fomu 34A kutoka vituo vya kupigia kura hadi IEBC Public Portal. (Kauli moja Koome, Mwilu, Ibrahim, Njoki, Wanjala, Lenaola, Ouko).

Hakukuwa na tofauti kubwa kati ya Fomu 34A zilizopakiwa kwenye Tovuti ya Umma ya IEBC na Fomu 34A zilizopokelewa katika Kituo cha Kitaifa cha Kujumlisha, na Fomu 34A zilizotolewa kwa Mawakala katika Vituo vya Kupigia Kura. (Kauli moja Koome, Mwilu, Ibrahim, Njoki, Wanjala, Lenaola, Ouko).

Kuahirishwa kwa Uchaguzi wa Ugavana katika Kaunti za Kakamega na Mombasa, uchaguzi wa Wabunge katika Majimbo ya Kitui Vijijini, Kacheliba Rongai na Pokot Kusini na wadi za Nyaki Magharibi katika Jimbo la Imenti Kaskazini na Kwa Njenga katika Embakasi Kusini hakujasababisha kukandamizwa kwa wapiga kura na kuwadhuru Raila Odinga. (Kauli Moja Koome, Mwilu, Ibrahim, Njoki, Wanjala, Lenaola, Ouko).

Hakukuwa na tofauti zisizoelezeka kati ya kura zilizopigwa kwa wagombea wa urais na nafasi zingine za uchaguzi. (Kauli Moja Koome, Mwilu, Ibrahim, Njoki, Wanjala, Lenaola, Ouko).

IEBC ilitekeleza uthibitishaji, kujumlisha, na kutangaza matokeo kwa mujibu wa Kifungu cha 138 (3) (c) na 138 (10) cha Katiba. Mamlaka ya kujumlisha na kuthibitisha si kwa mwenyekiti wa IEBC bali tume. Makamishna wanne walishiriki katika kujumlisha hadi dakika ya mwisho. (Kauli Moja Koome, Mwilu, Ibrahim, Njoki, Wanjala, Lenaola, Ouko).

Rais Mteule aliyetangazwa alipata kura 50%+1 ya kura zote zilizopigwa kwa mujibu wa Kifungu cha 138 (4) cha Katiba. Kura zilizokataliwa haziwezi kutumika katika hesabu ya kiwango hiki cha kikatiba. (Kauli Moja Koome, Mwilu, Ibrahim, Njoki, Wanjala, Lenaola, Ouko).

Hakukuwa na dosari na uvunjaji sheria wa kiwango cha juu kiasi cha kuathiri matokeo ya mwisho ya Uchaguzi wa Rais. (Kauli moja Koome, Mwilu, Ibrahim, Njoki, Wanjala, Lenaola, Ouko).
Kuhusu afueni na maagizo: William Ruto alichaguliwa kihalali. (Kauli moja Koome, Mwilu, Ibrahim, Njoki, Wanjala, Lenaola, Ouko).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!