March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hukumu ya Sheikh Ponda yakwama

Sheikh Ponda Issa Ponda

Spread the love

MAHAKAMA ya Rufaa imeshindwa kutoa hukumu ya rufaa ya Serikali dhidi ya Sheikh Issa Ponda baada ya jaji kutokamilisha kuiandika, anaandika Faki Sosi.

Katika rufaa hiyo Serikali inapinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro iliyomuachia huru Sheikh Ponda katika tuhuma ya uchochezi.

Hukumu hiyo iliyitarajiwa kutolewa leo na Jaji Mkasi Mongwa ambaye amesema ameshindwa kutoa hukumua hiyo kwa kuwa hajamaliza kuianda na badala yake ataitoa Tarehe 16 Novemba mwaka huu.

Inatarajiwa kwenye hukumu hiyo endapo Jaji Mongwa anayesikiliza shauri hilo ataridhika na madai ya upande wa Serikali, Sheikh Ponda atatiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu.

Kama Jaji hataona ukweli katika madai ya Serikali, atatupilia mbali rufaa hiyo na kumuachia huru Sheikh Ponda.

error: Content is protected !!