Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Hukumu ya Mdude kutolewa Leo
Habari za Siasa

Hukumu ya Mdude kutolewa Leo

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema, akisalimiana na Mdude Nyagali alipohudhuria kesi yake katika mahakama ya Mbeya
Spread the love

 

HUKUMU ya kesi ya Jinai Na. 36/2020, inayomkabili kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, inatolewa leo Jumatatu, tarehe 28 Juni 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa Jumatatu ya tarehe 14 Juni 2021, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Zawadi Laizer, lakini iliahirishwa.

Hakimu Laizer alisema, ameahirisha kusoma hukumu hiyo, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Wafuasi wa Chadema waliohudhuria kesi ya Mdude

Wakili wa Mdude, Faraji Mangula, alisema hukumu hiyo haikusomwa kwa kuwa haikuwa tayari.

Kada huyo wa Chadema anayesota rumande tangu Mei 2020, anakabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin, zenye uzito wa gramu 23.4.

Mdude alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, tarehe 10 Mei 2021, baada ya kufanyiwa upekuzi katika hoteli moja jijini humo, alikokuwa amepanga, na kudaiwa kukutwa na dawa hizo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!