March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hukumu kesi ya ‘Scorpion’ kusomwa mwakani

Salum Njwete (Scorpion)

Spread the love

HUKUMU ya kesi ya kumjeruhi mpaka kumtoboa macho kinyozi, Said Mrisho inayomkabili mwalimu wa sanaa ya kujihami, ‘Martial Arts’ na msanii wa filamu za kibongo, Salum Njwete (Scorpion) inatarajiwa kusomwa Januari 10 mwaka 2018, anaandika Hamis Mguta.

Kesi hiyo iliendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, ambapo Scorpion alikuwa akiulizwa maswali na wakili wa utetezi, Nassoro Katuga kufuatia utetezi wake alioutoa kipindi kilichopita akiongozwa na wakili wake, Juma Nassoro.

Katika utetezi wake wa awali Scorpion amesema alishurutishwa kutoa maelezo katika kituo cha polisi cha Buguruni ambapo wakili Katuga alimuuliza kwanini alisaini.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Flora Haule aliifunga kwa kuahidi kuitolea hukumu Januari 10 mwakani ambapo kabla ya hukumu hiyo kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Desemba 27 mwaka huu.

error: Content is protected !!