July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hukumu kesi ya Kubenea, Makonda Machi 3

Spread the love
HUKUMU ya Kesi inayomuhusu Saed Kubenea, Mbunge wa Jimbo la Ubungo pia Mkurugenzi wa Hali Halisi Publishers na Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kindononi itatolewa tarehe 3 Machi mwaka huu, anaandika Faki Sosi.
Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu Kisutu amesema, kesi hiyo itatolewa hukumu siku hiyo iwapo Kubenea atakuwa na kesi ya kujibu ama la na kwamba pazia la mashahidi limefungwa rasmi leo.
Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya viongozi hao wawili kugombana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam tarehe 14 Desemba mwaka jana ambapo Kubenea alikamatwa na polisi kwenye eneo hilo kwa amri Makonda .
Tukio hilo limetokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda hicho ambao walimpigia mbunge wao aende kutatua mgogoro huo ambapo Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana na kukutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu.
Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.
Ilipofika saa 10:30 Makonda alifika na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi.
Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na Waziri wa Afya Wanawake, Jinsia na Watoto.
Baada ya kutoa maagizo hayo, Makonda alimzuia Kubenea kuhutubia na kuaga wananchi aliokuwa nao tangu mchana, kutokana na hali hiyo (Kubenea) alisema ni vema aseme neno, ndipo mvutano ulipoanza.
Makonda alimuru mkutano ufungwe lakini wafanyakazi hawakutawanyika eneo hilo, alipoona hivyo aliamrisha Polisi wamkamate Kubenea ambapo sintofahamu iliongezeka.
error: Content is protected !!