Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Hukumu bosi Jamii forums Novemba 17
Habari Mchanganyiko

Hukumu bosi Jamii forums Novemba 17

Maxence Melo
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirisha kutoa hukumu ya kesi namba 458 ya mwaka 2016  inayomkabili Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo na mwenzake ya kuzuiya  Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Leo Ijumaa tarehe 30  Oktoba 2020, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi, amesema  hukumu ya kesi hiyo haijawa tayari hivyo amepanga 17  Novemba 2020 ndio siku ya kutoa hukumu juu ya shauri hilo.

Mshitakiwa mwengine kwenye shauri hilo ni Mwanahisa mwenzake, Melo Mike Mushi ambaye wameshtakiwa pamoja.

Kwenye shauri hilo, mabosi hao wa Jamii forums wanashitakiwa kuendesha Mtandao wa Jamii Forum bila kutumia kikoa cha Tanzania mathalan;-www.habari.tz).

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuzuia jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, kinyume na Sheria Namba 22 (2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandano Namba 14 ya mwaka 2015.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Aprili Mosi, 2016 na 13 Desemba  2016 katika maeneo ya Mikocheni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mchina wa SGR aburuzwa kortini kwa kumjeruhi Mtanzania, TRC waja juu

Spread the love  RAIA wa China, Zheng Yuan Feng, amefikishwa mahakamani kwa...

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

error: Content is protected !!