Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Hujuma za uchaguzi zatua bungeni
Habari za Siasa

Hujuma za uchaguzi zatua bungeni

Bunge la Tanzania
Spread the love

HUJUMA zinazofanywa na wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa, zimetua bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Baadhi ya wabunge leo tarehe 5 Novemba 2019, wamelitaka Bunge la Jamhuri kusimamisha shughuli zake na kujielekeza katika kujadili sintofahamu inayoendelea nchini kuhusu zoezi hilo.

Wabunge hao, hususani kutoka vyama vya upinzani, wamemwomba Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge kujadili ukakasi huo, hata hivyo spika hakutoa nafasi.

Maftaha Nachuma, Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini amelieleza Bunge, kwamba anashangazwa na wasimamizi wa uchaguzi kupuuza agizo la Suleiman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Kutokana na malalamiko pia kanuni na taratibu kuvunjwa, Waziri Jafo aliagiza wagombea walioondolewa kwa hila, warejeshwe.

Maftaha amelielekza Bunge, kwamba upinzani una vielelezo mbalimbali kuthibitisha kanuni na taratibu za uchaguzi huo kwenye hatua ya awali ‘zimebakwa’.

Mbunge huyo amemweleza Dk. Tulia, kwamba kama Bunge litaridhia, yupo tayari kukabidhi vielelezo hivyo kwa Job Nduga, Spika wa Bunge.

Anatropia Theonist, mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema, amelalamika hatua ya vyama vya upinzani kufinyangwa nchi nzima.

Amelieleza Bunge kwamba, mambo wanayofanyiwa vyama vya upinzania nchini hayastahili, na kwamba hatua ya Waziri Jafo kutoa kauli ya kutaka walioenguliwa kwa hila, warejeshwe ni kielelezo cha kilio chao.

Frank Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma ameonesha hofu yake kutokana na wasimamizi kukiuka kanuni na taratibu kwa makusudi.

Amesema, hatua hiyo inaweza kusababisha sintofahamu nchini ikiwa ni pamoja na machafuko. Ameitaka serikali kuwa makini ili kudumisha amani.

Akijibu hoja hiyo, Dk. Tulia amesema, tayari mamlaka husika zinashughulikia changamoto hiyo kwa kuwa, Waziri Jafo ametoa maelekezo.

Malalamiko ya kuumizwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, tarehe 24 Novemba 2019 yametolewa na vyama mbalimbali vya upinzani.

Miongoni mwa vyama vilivyotoka hadharani na kulalamikia hujuma hizo ni pamoja na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, Chama cha Umma (Chauma) na Chama cha ACT-Wazalendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!