April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hujuma Serikali za Mitaa: Chadema wamvaa Jafo, Msajili

Spread the love

MAZINGIRA mabovu, vitimbi na hujuma katika siku ya kwanza ya kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali, kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, yameitibua Chadema. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa za viashiria vya kuvurugwa uchaguzi huo, unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2019 kutoka maeneo mbalimbali nchini, zimekuwa zikiripotiwa.

Kwenye taarifa hizo, wanaolalamikiwa ni wasimamizi wa uchaguzi pia maofisa wa serikali ambapo wamekuwa wakitoa maelezo ya kukamata wapinzani, wengine kupigwa na hata kunyang’anywa fomu zao.

Taarifa ya Chadema, iliyotolewa na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya chama hicho imeeleza, imemwandikia barua Seleman Jaffo, Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Msajili wa Vyama vya Siasa na Ofisi ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzania bungeni kuhusu kadhia hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 30 Oktoba 2019, wamemtaka Jafo kuchukua hatua kuhusu ukiukwaji huo, kwa madai kwamba ni kiashirio cha kuvuruga na kuharibu uchaguzi huo.

“Kufuatia matukio yanayoonesha mazingira ya kuharibu uchaguzi wa serikali za mitaa yaliyojitokeza siku ya kwanza ya kuchukua, kujaza na kurejesha fomu za uteuzi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, siku ya Jumanne Oktoba 29, 2019,” aimeeleza na kuongeza;

“Chadema kimemwandikia barua Waziri Jafo, kumtaka achukue hatua za haraka dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi huo.”

Barua hiyo imeambatanishwa na taarifa inayoonesha mifano mahsusi kuhusu ukiukwaji huo wa kanuni,.

Miongoni mwa malalamiko ya Chadema ni wasimamizi na wasaidizi wa uchaguzi kutoa nakala za fomu zisizokuwa na nembo ya halmashauri na mhuri husika ili kuthibitisha kuwa ni nakala halisi, kutofunguliwa kwa ofisi kwa ajili ya kutoa fomu za kuomba kuteuliwa kugombea.

“Wasimamizi hao kutoa nakala za fomu za kuomba kugombea bila kuambatanisha fomu za maadili ya uchaguzi, jambo ambalo linaashiria kuweka mazingira ya kuwaengua wagombea wa Chadema. Wasimamizi kukataa kutoa fomu kwa sababu ambazo ni kinyume na kanuni,” imeeleza taarifa hiyo.

error: Content is protected !!