BENKI ya NMB nchini Tanzania, imezindua huduma ya Teleza Kidigitali na NMB MshikoFasta yenye lengo la kumuwezesha mteja kufungua akaunti mara moja na kuunganishwa na huduma mbalimbali za benki hiyo bila ya mahitaji ya vigezo vya usajili katika mkoa wa Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Wakizungumza wakati wa uzinduzi huo mjini hapa, leo Alhamisi tarehe 26 Mei 2022, wakazi wa Manispaa ya Morogoro wamesema huduma hiyo itasaidia kuwainua wafanyabiashara wadogo waodogo kwa lengo la kukuza mitaji biashara baada ya kujiunga.

Fundi wa kushona nguo mtaa wa Masika, Jeni Ndembeka amesema huduma hiyo mpya ya Teleza Kidigitali kwa namna inavyoelezwa na maafisa wa benki hiyo inaonyesha wafanyabiashara watakuja kunufaika na huduma hiyo kutokana na urahisi wake kuitumia.
“Hii huduma nimeona imelenga kuwawezesha wafanyabiabiashara kupata mitaji midogomidogo hasa wenye biashara ndogo ndogo ili kunufaika zaidi kwa kukuza mitaji yetu na unaweza kulipa ada ya wanafunzi na kulipa kwa njia rahisi bila kwenda ofisi za benki yao ya NMB,”alisema Ndembeka.
Mfanybiashara wa viungo vya mboga soko kuu la Chief Kingalu, Asia Mohamed alisema ujio wa huduma hizo mpya za NMB Pesa wakala, Lipa Mkononi na MshikoFasta ameona zinarahisisha utunzaji wa fedha za mauzo lakini na mifumo ya kukopa fedha imekuwa urahisi zaidi.
“Ufunguaji wa akaunti kupitia hii huduma ya Teleza Kidigitali naona ina faida katika upande wa kukopa fedha na kulipa kwa njia ya simu inatoa fursa kwa mfanyabiashara kutopoteza muda ambao angefanya mambo mengine na imekuwa rahisi hata wanaotunza fedha katika kibubu watashawishika kutunza fedha benki,” alisema Asia.
Mfanyabiashara mwingine katika soko hilo, Cleophas Kalega alisema Teleza Kidigitali inawezesha mteja wa benki ya NBM kukopa fedha kuanzia Sh.5,000 hadi Sh.500,000 kwa njia ya simu.
“Kwa namna nilivyopata maelezo ya hawa NMB ni kuwa mteja wao aliyejiunga na huduma hii ya Teleza Kidigitali na NMB Pesa maana yake ana uwezo wa kukopa fedha kuanzia Sh.5,000 hadi Sh.500,000 katika simu kwa kadiri unavyokopa na kulipa kwa wakati unafikia kiwango chao cha juu cha Sh.500,000 mfanyabiashara atakopeshwa,” amesema Kalega.
Akizungumzia huduma hiyo wakati wa uzinduzi Masika mjini Morogoro, Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema kampeni ya Teleza Kidigitali imewalenga watanzania kuwapunguzia mlolongo wa kupoteza muda kufuata huduma za kifedha katika taaisis za fedha hapa nchini.
Mlozi alisema watanzania wengi hawana mwamko wa kutumia taasisi za fedha kwa ajili ya kutunza, kupata mitaji na kukopa fedha umekuwa mdogo na wao kama NMB wanaendelea kuboresha mifumo teknolojia kuwafikia wateja wao kupata mikopo bila urasimu.
“Kampeni ya Teleza Kidigitali ilizinduliwa rasmi April na waziri mkuu Dodoma na leo tunazindua mkoa wa Morogoro hapa Masika na huduma ya NMB mkono nayo imeboresha kupitia njia ya simu na hii inasaidia kuwapunguzia muda wateja wetu ambapo wilaya zote za mkoa huu timu ya kampeni hii itawafikia,” amesema Mlozi.
Leave a comment