May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Huduma ya luku majanga, Tanesco yaomba radhi

Spread the love

 

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema, huduma ya manunuzi ya luku kwa njia ya mtandao, inatarajia kurejea leo Jumatatu, tarehe 7 Juni 2021, kuanzia saa 12:00 jioni. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Ni baada ya kuadimika kwa saa kadhaa na kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaotafuta huduma hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Tanesco imesema, kukosekana kwa huduma hiyo ni “hitilafu iliyobainika wakati wa maboresho yanayoendelea katika mfumo wa manunuzi ya Luku.”

“Tanesco linawaomba radhi wateja wake kutokana na kukosekana huduma ya manunuzi ya umeme wa Luku kwa njia ya mtandao. Huduma hiyo, inatarajia kurejea leo Jumatatu, kuanzia saa 12:00 jioni,” imeeleza taarifa hiyo

Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, tatizo hilo linajitokeza na kusababisha baadhi ya mameneja wa kitengo hicho, kusimamishwa kupisha uchunguzi.

Waliosimamishwa kupisha uchunguzi ni; Meneja wa Tehama na Huduma za Biashara wa Tanesco, Lonus Feruzi na wasaidizi wake wawili, Frank Mushi na Idda Njau.

error: Content is protected !!